Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akizindua Bahati Nasibu
ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.
Kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho na
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James
Shigongo.
Paul Makonda akigawa vipeperushi vyenye nyumba na zawadi nyingine zinazoshindaniwa kwa wanahabari.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakichukua matukio.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo akiongea na
wanahabari kuhusu lengo la Global kuendesha shindano hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea na wanahabari (hawapo
pichani) kabla ya uzinduzi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kutoka
Global.
Wanahabari wakimsikiliza Paul Makonda.
Abdallah
Mrisho (wa pili kulia) akimkaribisha Paul Makonda (katikati) kuzindua
rasmi Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.
Wengine pichani ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Oscar
Ndauka (wa kwanza kulia), Mhariri Mtendaji wa Global Richard Manyota (wa
kwanza kushoto) na Eric Shigongo wa pili kushoto.
Wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja na Paul Makonda mara baada ya uzinduzi huo.
KAMPUNI
ya Global Publishers Ltd inayochapisha magazeti ya Uwazi, Ijumaa,
Championi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda yanayosambazwa nchi nzima,
imeandaa Bahati Nasibu kwa wasomaji wa magazeti yake ambayo inaanza
rasmi Ijumaa, Desemba 11, 2015.
JINSI
YA KUSHIRIKI Msomaji atatakiwa kununua nakala moja au zaidi ya magazeti
tajwa na kukata kuponi moja iliyomo ndani ya magazeti hayo. Atatakiwa
kujaza jina lake kamili na anwani yake na kisha kuituma kwa njia ya
posta au kuipeleka moja kwa moja katika ofisi za Global Publishers au
kwa mawakala wake waliyopo sehemu mbalimbali nchini. Kwa wale wa
mikoani, nao wanaweza kutuma moja kwa moja kwa mawakala wetu au kutuma
kwetu kwa njia ya posta.
Kutakuwa
na vituo vya kukusanyia kuponi katika kila kata na mitaa mbalimbali
nchini Tanzania. ZAWADI Bahati Nasibu hii inatarajiwa kuendeshwa kwa
muda wa miezi 6, tunatarajia kutoa zawadi ya nyumba mpya mwishoni mwa
mchezo huu ambayo imejengwa eneo la Salasala, Wilayani Kinondoni, jijini
Dar es salaam, nyumba hiyo ni mpya kabisa na itakuwa na samani ndani na
hadi sasa imeshamilika kwa alilimia 95. Pia kutakuwa na Droo nyingine
ndogo kila mwezi zitakazotoa zawadi za Simu za Kisasa, Runinga na
Ving’amuzi vyake, na vyombo vya mbalimbali vya nyumbani.
MASHARTI
Wasomaji wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 wanaruhusiwa kushiriki,
lakini wafanyakazi wa Global Publishers, waandishi wake na ndugu zao
hawaruhusiwi kushiriki. Msomaji anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadri
awezavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi ya Nyumba na zawadi
nyingine.
Kuponi
zote zitaingia katika droo ndogo na kubwa. HISTORIA YA GLOBAL KATIKA
BAHATI NASIBU GLOBAL Publishers ni kampuni pekee ya uchapishaji wa
magazeti nchini ambayo imekuwa ikiandaa Bahati Nasibu na kutoa zawadi
kubwa kwa wasomaji wake mara kwa mara. Imekuwa ikiendesha Bahati Nasibu
mbalimbali kupitia magazeti yake tangu mwaka 2000 na kwa nyakati tofauti
imeshatoa jumla ya magari 5, kama vile Nissan March, Toyota Vitz,
Mitubish Pajero, Mercedes Benz na Toyota Noah na zawadi nyingine nyingi
za tahamani, ikiwemo kumpeleka msoamaji wake mmoja Hong Kong kutalii.
Global
Publishers imekuwa ikifanya yote haya si kwa sababu ina fedha nyingi
sana, bali inafanya haya kama njia moja wapo ya kuwashukuru wasomaji
wake kwa kuendelea kuyaamini na kuyasoma magazeti yake kwa zaidi ya
miaka 15 sasa, pia inafanya haya kama njia moja wapo ya kurejesha kwa
wasomaji sehemu ya kipato chake ili kuboresha maisha yao.
Aidha
inafanya hivi pia kwa ajili ya kuimarisha na kuongeza idadi ya wasomaji
wake. Mwisho, tunawahakikishia wasomaji wetu kuwa washindi wote wa
Bahati Nasibu za Global publishers hupatikana kihalali chini ya
usimamizi madhubuti wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha na
huchezeshwa kwa wazi kila mtu akiona.
Tunakushukuru
sana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda kwa kuja kuizindua
rasmi Bahati Nasibu hii na tunakupongeza kwa kazi yako nzuri kwa taifa.
Asante Meneja Mkuu, Global Publishers Ltd.
No comments:
Post a Comment