HOSPITALI ZA APOLLO MSTARI WA MBELE KUOKOA MAISHA YA WAHANGA WA MAFURIKO MJINI CHENNAI - LEKULE

Breaking

11 Dec 2015

HOSPITALI ZA APOLLO MSTARI WA MBELE KUOKOA MAISHA YA WAHANGA WA MAFURIKO MJINI CHENNAI

Preetha Reddy, Makamu Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo,

Na Mwandishi Wetu,
CHENNAI ni jiji la tano kwa ukubwa nchini India, jiji hilo limepigwa na janga kubwa la mafuriko ambayo hayajawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, mafuriko hayo yameliacha jiji hilo likiwa hoi na taabani. 

Mafuriko hayo ya kihistoria yalisababisha jiji hilo kukosa huduma muhimu kama umeme, maji safi, chakula, usafiri na mahitaji mengine ya msingi. Idadi ya wagonjwa wengi wameripotiwa kufariki baada ya maji ya mvua kubwa kuharibu majenereta na mfumo mzima wa umeme kwenye hospitali mbalimbali mjini humo.

Kufuatia mafuriko hayo makubwa jiji Chennai, hospitali za Apollo zilizopo Chennai zimeripotiwa kuwa zinaendelea kufanya kazi vizuri na kuwa mstari wa mbele kutoa huduma kwa waathirika wote wa hayo mafuriko. Wakati hospitali nyingi Chennai zikiwa zinasumbuka na tatizo la umeme; hospitali za Apollo zina endelea kutoa huduma bora na kuzidi kutumia timu yao ya wataalamu waliojikita katika kuokoa maisha ya watu wengi.

Preetha Reddy, Makamu Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo, alisema wametenga timu 30 zenye wataalamu wa afya kama 300 katika kukabiliana na wahanga hao wa mafuriko.

Kwa mujibu wa N. Sathyabhama, mkurugenzi wa huduma za afya na ubora wa kanda ya kaskazini katika hospitali za Apollo; hospitali ya Apollo imepokea wagonjwa wengi kutoka hospitali nyingine nyingi mbalimbali zilizokumbwa na ukatikaji wa umeme kutokana na mafuriko.

Mwendelezo wa huduma kutoka hospitali za Apollo katika sehemu mbalimbali jijini umesababisha wagonjwa kutohamishiwia hospitali nyingine, licha ya kupokea zaidi ya wagonjwa 50 ambao wengine ni wageni nchini India kutoka hospitali nyingine zilizoathirika na janga hilo, alisema.

Wagonjwa ambao ni wageni nchini India kutoka nchi zaidi ya 20 waliokuwepo hospitali za Apollo walipewa kadi ya mawasialiano ya ISD na huduma ya mtandao ili waweze kuwasialiana na familia zao, alisema Dk. Srinidhi Chidambaram makamu wa Rais wa idara ya wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali. Ndugu Ahmed Noumani kutokea Oman amedhibitisha kuwa ameona ubinadamu wa ukweli kutoka hospitali za Apollo, alijisikia yupo salama na mwenye ulinzi mzuri na pia kuwezeshwa kuwasiliana na familia yake muda wote iliyopo nchi ya Oman.

Ongezeko kubwa la kiwango cha maji kwenye mabwawa ilipelekea mto Adyar kufurika na kuleta majanga jijini na vijijini. Alisema umeme ulikatika kwa muda wa masaa 57 katika jengo moja na masaa 69 jengo lingine lakini waliendelea kufanya kazi kwa kutumia jenereta. Kwa ajili ya usalama, umeme ulikatwa kwa siku kadhaa jijini Chennai na maeneo ya jirani yake.

“Tunatoa kipaumbele katika huduma kwa wagonjwa. Ni yale matibabu ya dharura tu na matumizi ya vifaa vya uokoaji ndivyo tulivyoshungulika navyo. Kipaumbele kilikuwepo zaidi katika maeneo yaliyoathirika sana,” alisema Bi. Sathyabhama

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, ukatikaji wa umeme ulifanyika kuanzia Ijumaa wiki iliyopita kwa sababu za kiusalama.

Kufuatia mvua kali zinazoambatana na upepo nchini India katika mji wa Tamil Nadu, hospitali za Apollo zimetoa huduma bure za afya na kuweka vituo na kambi za matibabu kwa wahanga wote jijini Chennai.

Kambi iliwekwa katika ofisi ya baraza kuanzia saa tatu asubuhi. Timu ya madkatari 20 inayojumuisha wataalamu wa magonjwa ya tumbo (gastroenterologists), madaktari wa kawaida, wataalamu wa magonjwa ya watoto (paediatricians),wataalamu wa magonjwa ya wanawake (gynaecologists), wataalamu magonjwa ya shingo na kichwa (ENT specialists),wataalamu wa uti wa mgongo na misuli (orthopaedicians), na wataalamu wa magonjwa ya mapafu (pulmonologists) wakiwa na manesi 20 na matabibu wengine kutoka Hospitali za Apollo waliwekwa kwenye hizo kambi.



Hospitali za Apollo zimetoa mchango mkubwa sana katika kuokoa maisha ya wananchi wengi wa India katika kipindi hiki cha mvua za mafuriko jijini Chennai. Magwiji hao wanaongoza kwa huduma bora za afya ulimwenguni wameonyesha mfano wa kuigwa wa namna vituo vya afya vinatakiwa kuwa bora na msaada katika kuokoa maisha hasa pale majanga yanapoteka

No comments: