Wakuu wa Mikoa na Wilaya Dhibitini Migogoro Ya Ardhi – Waziri Mkuu - LEKULE

Breaking

24 Dec 2015

Wakuu wa Mikoa na Wilaya Dhibitini Migogoro Ya Ardhi – Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanaongeza udhibiti na usimamizi wa migogoro ya  ardhi kwenye maeneo yao husika.
 
Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Desemba 23, 2015) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi kwenye Ikulu ndogo mara baada ya kuwasili akitokea jimboni kwake Ruangwa.

“Ardhi ni mali ya Serikali lakini maeneo yanayotwaliwa kwa sababu mbalimbali za maendeleo yasiwe chanzo cha migogoro na wananchi tunaowaongoza,” alisema.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema anatambua kuna mgogoro wa eneo la mgodi katika wilaya ya Ruangwa baina ya wananchi na wawekezaji wa kampuni ya Uranex. .....
"....Na hii ni kwa sababu wao ndiyo waliamua kufanya tathmini (evaluation) ya eneo hilo. Yale ni makosa kwa sababu aliyepaswa kufanya tathmini ni Halmashauri na siyo mwekezaji,” alisema.

Alisema wawekezaji wanaruhusiwa kisheria kufanya tathmini lakini sheria waliyoitumia ni sheria namba 8 peke yake. “Kama Halmashauri ingefanya kazi hiyo ni lazima wangetumia sheria ya ardhi ya vijiji pamoja na sheria ya madini na wananchi wangepata thamani halisi ya ardhi yao,” alisema.

“Ninaagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ikahakiki lile eneo na kubaini kama ni la kilimo au la madini na kama ni la kilimo, wananchi wamelima mazao gani na kwa muda gani kisha wafanye tathmini upya. Yuko valuer wa Halmashauri mwenye dhamana hiyo na siyo wao,” alisema.


“Nasisitiza tena ni vema Wakurugenzi wote, Wakuu wa Wilaya chini ya uongozi wa Wakuu wa Mikoa mjiridhishe kuwa hakuna migogoro kwenye maeneo yenu. Kama ipo, imalizeni kwa kukaa mezani na kuzungumza na pande husika, inawezekana kabisa,” alisisitiza.

No comments: