Mkulima
mmoja ameuawa, mwingine amejeruhiwa wakiwemo askari polisi wawili
kwenye mapigano dhidi ya wafugaji wa kimang’ati kwenye kijiji cha
Dihimba Turiani, mkoani Morogoro.
Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa amesema mapigano hayo yametokea
baada ya wafugaji kutaka kuwachukua kwa nguvu ng’ombe zaidi ya 150
waliokuwa wakishikiliwa na wakulima kwenye ofisi ya kijiji hicho.
Mkwasa
amesema siku ya tarehe 11 mwezi huu, mkulima mmoja aliyejulikana kwa
jina la Bakari Mulunguza alikuta ng’ombe zaidi ya 150 wakila shambani
kwake pasipo kuwa na mchungaji wa ng’ombe hao, ndipo Mulunguza alipoomba
msaada kutoka kwa wakulima wenzake kwa pamoja waliwaswaga ng’ombe hao
hadi kwenye ofisi ya serikali ya kijiji.
Amesema
wakulima hao waliamua kuchukua uamuzi huo ili mwenye ng’ombe ajitokeze
na kupigwa faini kutokana na uharibifu uliosababishwa na ng’ombe hao.
Alisema siku iliyofuata ya tarehe 12, ndipo alipojitokeza mfugaji mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Shaabani Ikeli na kudai kuwa yeye ndiye
mmiliki wa ng’ombe hao.
“Serikali
ya kijiji ilimtaka mfugaji huyo kulipa faini ya Shilingi laki mbili
kama fidia kutokana na uharibifu uliosababishwa ; mfugaji huyo alikubali
na kuahidi kuwa angelipa faini hiyo, lakini cha kushangaza alirudi na
kundi kubwa la vijana wafugaji wakitaka kuwachukua ng’ombe kwa nguvu,
ndipo mapigano yalipotokea,” alisema Mkwasa.
Alimtaja
aliyeuawa kuwa ni Mohamed Musa (43) mkulima wa kitongoji cha Kaole, na
aliyejeruhiwa ni Charles Paulo (35) ambaye amelezwa hospitali ya Bwagala
Turiani kwa matibabu.
Mkwasa
amesema kitendo hicho kiliamsha hasira kwa wakulima ambao walilipa
kisasi kwa kuwakatakata miguu na sehemu mbalimbali za miili ng’ombe 150.
Alisema polisi walifika eneo la tukio na kudhibiti vurugu hizo; amesema
polisi wawili wamejeruhiwa kweye mapigano hayo.
Mwigulu Nchemba Afika Afika Eneo La Tukio
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji Mh. Mwigulu Nchemba leo hii amefika katika eneo la tukio.Akizungumza na wananchi hao Waziri Nchemba alikuwa na haya ya kusema;
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji Mh. Mwigulu Nchemba leo hii amefika katika eneo la tukio.Akizungumza na wananchi hao Waziri Nchemba alikuwa na haya ya kusema;
"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, hakuna ardhi au mnyama mwenye thamani sawa na maisha ya mwanadamu yeyote yule,njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakulima na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na uongozi wa serikali wa eneo husika hatua kwa hatua".
Pia Mh. Mwigulu amesema ameagiza ulinzi maeneo yote yenye migogoro, pili wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia na kwa walio jeruhiwa, ameagiza wapatiwe matibabu kwanza bila kuchelewa na hatua za kisheria kwa wenye hatia zifuate.
"Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi, tunakwenda kuunda kamati za usuluhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria."
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment