JUMLA
ya Asasi 45 zinazofanya kazi na wafugaji wa asili kuhusu migogoro ya
ardhi Tanzania, wamelaani na kutoa tamko la kuitaka serikali
kuwawajibisha watumishi wote wa serikali na baadhi ya viongozi wa dini
ambao wanasababisha kuwepo kwa migogoro ya ardhi nchini na kusababisha
watu kupoteza maisha na mifugo kuuliwa.
Katika
tamko hilo lililosomwa katika mkutano wa wadau wa programu ya wafugaji
wa asili Tanzania na Mkurugenzi wa Shirika la Cedesota, Jackson Muro
amesema migogoro mingi imekuwa ikifanywa na watumishi wa serikali au
viongozi wa dini kutokana na kutokuwa waaminifu kwa kutaka rushwa.
Kwenye
tamko hilo Muro amesema kwa kauli moja washiriki hao wanaitaka serikali
kuwajibika kwa kuhakikisha wanakabiliana kwa haraka na tatizo hilo
jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa migogoro isiyoisha.
Amesema
migogoro mingi ya ardhi haiwaathiri tu wafugaji pekee bali inayakumba
makundi mengine na kusababisha kuwepo kwa matatizo mengine.
Alivitaja
vyanzo vya migogoro hiyo amesema kuwa ni Sheria ya utambuzi wa mifugo
2010 kuanzia uhamiaji wa wafugaji wa asili na mifugo, Sheria ya
wanyamapori 1998 inazuia uhamiaji wa wafugaji katika maeneo ya
wanyamapori ilihali maeneo mengi yanayofaa kwa malisho yakitwaliwa kwa
ajili ya uhifadhi.
Walitaja
sababu nyingine ambazo zinasababisha migogoro ni pamoja na Sheria ya
hifadhi ya mazingira ya Mwaka 2007 inaainisha kuwa ufugaji wa asili ni
moja ya vyanzo vya uharibifu wa mazingira jambo linalopotosha jamii na
kusababisha migongano baina ya wafugaji asili, Mamlaka husika na makundi
mengine, licha ya kwamba ufugaji asili ni rafiki wa mazingira.
Alisema
kutokana na kuwepo kwa migogoro ya ardhi hiyo kunapelekea watu kuuwawa
huku mifugo nayo ikiuwawa jambo ambalo linasababisha umasikini.
“Migogoro
ya ardhi imesababisha kuwepo kwa vifo vingi vya watu mifugo, majeruhi
na ulemavu wa kudumu, uharibifu wa mali na mazao mashambani, kuzorotesha
shughuli za uzalishaji mali kutokana na hofu miongoni mwa wanajamii,
umasikini, visa na chuki miongoni mwa jamii, ubakaji na vingine vya
ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na uharibifu wa makazi,” alisema Muro.
“Kutokana
na kuwepo kwa matukio hayo umoja huo taasisi zisizo za kiserikali
tunachukua hatua hii kulaani, vitendo vya uvunjifu wa amani ,haki za
kibianadamu na za wanyama vilivyojitokeza wilayani Mvomero na Kilosa
Mkoani Morogoro Desemba 14 mwaka huu vilivyopelekea vifo watu na mifigo.
“Kwa
kauli moja tunatoa tamko la kuitaka serikali iwajibike na kumtaka
waziri ardhi kubainisha na kuweka wazi maeneo yote ya wafugaji
yaliyoodhiwa na wawekezaji wasio rasmi na wasio rasm ili yarejeshwe kwa
wafugaji.
“Serikali
kwa kushirikiana na wadau iwe mkakati wa pamoja wa kuelimisha Umma juu
ya umuhimu wa amani baina ya makundi yote katika jamii na kulinda haki
ya kila mmoja,” lilisema tamko hilo lenye mambo 8.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Katibu mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo
na Uvuvi, Anociata Njombe alikiri kuwepo kwa mgogoro wa ardhi kwa muda
mrefu ambao kwa sasa unatafutiwa suluhisho na serikali ya awamu ya tano.
“Pamoja
na ukweli kwamba ufugaji ni shughuli ya kiuchumi kwa hapa nchini bado
lipo pengo la kisera katika kukidhi malengo na mahitaji halisi ya
kuboresha ufugaji wa asili,” alisema.
Alisema
ni kweli wafugaji wanaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo
za ukosefu wa maeneo ya malisho kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Alisema
kuna changamoto nyingine ambayo ni ukosefu wa malisho na maji, magonjwa
ya mifugo na ukosefu wa huduma za jamii katika maeneo ya wafugaji
asili.
“Changamoto
hizi zimezidi kuongezwa makali na kasi ndogo ya mipango ya matumizi ya
ardhi na kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji,” alisema Njombe.
No comments:
Post a Comment