Zogo
kubwa liliibuka katika kikao cha kuwachagua Meya na Naibu Meya wa
Manispaa ya Dodoma jana. Zogo hilo lilisababisha viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuzichapa
kavukavu.
Hali
hiyo ilitokea wakati wa kuapisha madiwani 56 na kufanya uchaguzi katika
Viwanja vya Ukumbi wa Manispaa hiyo mjini Dodoma, ilisababishwa na
lugha za vijembe na kashfa kati ya vyama hivyo viwili.
Vurugu
hizo zilizodumu kwa takribani dakika 20 ziliwakutanisha ana kwa ana
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Dodoma, Aifraim Kolimba (CCM) na
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Dodoma, Vicent Emmanuel ambao
walikunjana.
Viongozi hao walikunjana kwa dakika kadhaa kabla ya mgambo wa Manispaa kuwatenganisha na kuwatuliza.
Pamoja
na mgambo hao kurejesha hali ya utulivu, makada hao waliendelea
kurushiana matusi ya nguoni huku kila mmoja akikashifu chama cha
mwenzake.
Tukio
hilo lilikoma mara baada ya Diwani wa Kata ya Kizota (Chadema), Jamal
Yaled alipowataka makada na viongozi wa chama chake kutulia. “Jamani wala msipigane, hawa tutawanyoosha katika Baraza nawaomba mtulie,” alieleza Yaled.
Kuwasili
kwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, FFU, kulifanya vurugu
iliyokuwepo awali kutulia na shughuli za uchaguzi kuendelea.
Katika
uchaguzi huo, madiwani 48 kati ya 56 walimpitisha Japhary Mwanyemba
kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa asilimia 82, huku Naibu Meya akichaguliwa
Jumanne Ngede.
Akitangaza matokeo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Clemence Mkusa alisema, “Namtangaza kwenu Jumanne Ngede kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma kwa kura 48 kwa asilimia 82 kama za Mwanyemba."
Akizungumza
baada ya kuchaguliwa, Mwanyemba aliwataka madiwani hao kuvunja makundi
kwa kuhakikisha wanatetea matatizo ya wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment