Louis Van Gaal.
Baada
ya kutoa sare na timu ya West Ham United, Kocha wa Manchester United,
Mdachi Louis Van Gaal amezungumzia nafasi ya timu yake kama inauwezo wa
kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya (UEFA Champion League).
Majibu
ya kocha huyo yalitegemewa na watu wengi kutokana na mwenendo ulivyo
kwa sasa kwa klabu hiyo kongwe ya nchini Wingereza ambayo imekuwa
inapata matokeo ambayo hayawaridhishi mashabiki wa timu hiyo, Van Gaal
amesema kikosi chake bado hakijawa na uwezo wa kutwaa ubingwa huo kwa
kulinganisha na timu zingine zinazoshiriki mashindano hayo.
“Sidhani kama tunaweza kushinda Klabu Bingwa kwa sasa labda kwa mwaka ujao kama tukijiimarisha katika kikosi chetu,
”
Tunaweza kuifunga kila timu tunayokutana nayo kwa sasa lakini bado
hatuna uwezo wa kushinda Uefa, lakini tutajaribu kufanya kila kitu tuone
itakuwaje,” alisema Van Gaal.
Aidha
Van Gaal amezungumzia mchezo wao wa jumanne wa Ligi ya Mabingwa dhidi
ya Wolfsburgya Ujerumani ambao ni mchezo muhimu kwao kupata matokeo
mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa hatua ya 16 bora.
“Tunaweza
kushinda jumanne, tunatengeneza nafasi kila mchezo na tutatengeneza
zaidi katika mchezo wa jumanne na tunahitaji kupambana ili kushinda
mchezo huo, tumecheza leo jumamosi, tunapumzika jumapili na jumatatu
tunasafiri ni ngumu kujiandaa zaidi lakini tutakabiliana na wapinzani,”
alisema Van Gaal.
No comments:
Post a Comment