Bendera ya muungano wa upinzani wakipeperusha bendera kwa furaha.
Tume ya
uchaguzi nchini Venezuela imethibitisha kwamba muungano wa upinzani
umeshinda wabunge tisini na tisa kati ya mia moja na sitini na saba
katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita kwa mbili ya
tatu ya kura zote zilizopigwa.
Ushindi
huo wa kishindo unaupa muungano wa kidemokrasia nguvu za kutosha
kukabiliana na rais mwenye mrengo wa kijamaa, Nicolas Maduro.
Hili
linajumuisha uwezo wa kubadili uteuzi wa nafasi za majaji wa mahakama
kuu nchini humo na hata ikibidi kuanzisha kura ya maoni endapo
watahitaji kufuta mamlaka ya Bw Maduro .
Muungano
huo wa kidemokrasia nchini Venezuela umesema kwamba vipaumbele vyake
pindi watakapoanza majukumu ya kuwatumikia raia wa nchi hiyo ni
kuwaachilia huru viongozi wote wa upinzani walioko jela, na kuunusuru
uchumi wa nchi hiyo ambao unakwenda kombo.
Ushindi
huo kwa upande wa upinzani unahitimisha utawala wa miaka kumi na saba
uliokuwa una hodhiwa na chama cha kijamii cha marehemu Rais Hugo Chavez.
No comments:
Post a Comment