Bunge la
Uingereza hii leo linatarajia kupiga kura kuiruhusu nchi yao kujiunga na
mapambano dhidi ya kundi la dola la kiisilamu la IS nchini Syria.
Waziri
mkuu wa Uingereza , David Cameron ambaye ari yake ya kuliangamiza kundi
hilo la dola la kiisilamu imeongezeka zaidi hasa baada ya mashambulizi
ya mjini Paris anatarajiwa kuongoza mjadala bungeni unaotarajiwa
kuchukua zaidi ya saa kumi katika kuelekea upigaji kura huo.
Mawaziri
nchi humo wanaimani kwamba wabunge watapiga kura ya ndiyo kuunga mkono
hatua hiyo hali ambayo inaashiria kuwa ndege za kijeshi za Uingereza
zitaanza mashambulizi kulilenga kundi hilo la dola la kiisilamu huko
nchini Syria kabla ya kufikia mwisho wa juma hili.
Cameron
amesisitiza ya kuwa hatua za kijeshi zinahitajika sasa ili kuzuia
mashambulizi kama yale ya yaliyoua watu 130 mjini Paris mwezi uliopita,
lakini pia akiongeza kuwa hatua hiyo itaenda sambamba na juhudi za
kidiplomasia zinazoendelea sasa katika kushughulkikia mgogoro wa Syria.
"
Nitajitahidi kujenga hoja na nina imani kuwa wabunge wengi kutoka katika
vyama vyote wataniunga mkono " alisema waziri mkuu Cameron katika
kuelekea kura hiyo:
Hata
hivyo baadhi ya wataalamu wa masuala ya kisiasa na ya kivita, wanasema
wabunge kadhaa na raia wa kawaida wanaonekana kuwa na mashaka. Makundi
ya watu wanaopinga mambo yanayohusiana vita tayari wameandamana
kuonyesha kutounga mkono hatua hiyo.
Baadhi ya
wachambuzi wanauona hatua hii ya uingereza kutaka kushirika katika
kampeni dhidi ya kundi hilo la dola la kiisilamu kama hatua moja wapo ya
kuwaunga mkono bega kwa bega washirika wake ambao ni mataifa ya
Marekani na Ufaransa.
" Cameron
kwa sasa anaona ni lazima aiunge mkono Ufaransa katika kipindi hiki
inachokabiliana na tatazo la ugaidi " alisema Ben Berry ambaye ni mmoja
wa washauri katika siasa za kimataifa.
Tayari
Uingereza imekuwa ikishiriki katika mashambulizi ya anga dhidi ya kundi
la dola la kiisilamu nchini Iraq kampeni ambayo ilianza tangu mwaka
jana.
Aidha
inaarifiwa pia kuwa Uingereza imeombwa nawashirika wake yakiwemo mataifa
ya Ufaransa na Marekani kujiunga kikamlifu katika kampeni hiyo ya
mashambulizi dhidi ya kundi hilo la dola la kiisilamu.
Tayari
kumekuwepo na maandamanao nchini humo kupinga hatua ya kivita dhidi ya
kundi hilo la dola la kiisilamu kama anavyosema mmmoja wa watu
walioshiriki katika maandamano hayo
Chama cha Labour chagawanyika kuhusiana na hatua
Hatua hii
ya Cameron inakuja mnamo wakati chama kikuu cha upinzani cha Labour
nchini humo kikiwapa uhuru wa kuamua wabunge wa chama hicho katika
kuunga mkono au kutounga mkono uamuzi huo pasipo shinikizo lolote
kutokana na msimamo wa kiongozi mkuu wa chama cha Labor Jeremy Corbyn
anayeonekana kupinga hatua hiyo .
"
Tunataka kuwaua watu nchini mwao kwa kutumia mabomu yetu , tafadhali
pigeni kura ya kutounga mkono hatua hii ya serikali dhidi ya
mashambulizi ya nchini Syria" alisema kiongozi huyo wa chama cha Labor
Hata
hivyo hatua hii ya kutopata shinikizo kutoka katika chama chao
inaonyesha kuwa wabunge wa chama cha Labour ambao wanataka hatua za
kijeshi zichukuliwe dhidi ya kundi hilo la dola la kiisilamu watapiga
kura ya ndiyo hali ambayo inaonesha kuwa waziri mkuu Cameron atapata
ushindi mkubwa katika azima yake hiyo.
Mwandishi: Isaac Gamba/AFPE
Mhariri :Gakuba Daniel
Chanzo:DW
No comments:
Post a Comment