King Kiki (kulia) akiimba sambamba na Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ enzi za uhai wake.
Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ akiwa na Issa Nundu (kulia).
Habari
zilizoufikia mtandao huu jana jioni zinaeleza kuwa mwanamuziki mkongwe
katika tasnia ya muziki wa dansi nchini mwenye asili ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ amefariki
dunia nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar.
Kwa
mujibu wa wanamuziki waliofanya naye kazi kwa muda mrefu, Kasongo ambaye
alifanya kazi na bendi nyingi kama Maquis du Ziare akiwika na Nyimbo za
Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na zingine
kibao amefariki dunia baada ya kuumwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na
Kisukari hivyo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake.
Katika
siku za mwishoni, Kasongo aliitumikia Bendi ya Bakulutu kabla ya
kujiunga katika Bendi ya Bana Maquis ikiwa chini ya Tshimanga Kalala
Asssosa.
No comments:
Post a Comment