Uchambuzi Mfupi Wa Habari Kuu; Uchafu Ni Bidhaa Tunayozalisha.. - LEKULE

Breaking

10 Dec 2015

Uchambuzi Mfupi Wa Habari Kuu; Uchafu Ni Bidhaa Tunayozalisha..


Ndugu zangu,

Imedhihirika, kuwa Watanzania wanaweza kubadilika. Na usafi ni mazoea, na mazoea hujenga tabia. Tuendelee sasa kujenga mazoea ya usafi kwenye miji yetu. Inawezekana.
Na uchafu ni bidhaa, tupunguze kuzalisha uchafu. Na bahati mbaya wakazii wa miji yetu hawajui takwimu za tani za bidhaa uchafu zinazalishwa kila siku.
Kuna kitu kinaitwa ' Waste Management', labda isemwe udhibiti wa bidhaa taka. Kitu hicho hatuna utamaduni nacho pia. Watu hawajui hata wapi watupe maganda yao ya ndizi au chupa tupu za maji.
Kwa mijini, tungeweza kuwa na utaratibu wa kila nyumba iwe na pipa lake la taka nje, lenye mfuniko. Iliwahi kuwa hivyo wakati sisi wa Kizazi cha Azimio tunakua.
Na kuwe na siku ya tatu za wiki, gari la taka lipite kusomba taka hizo.
Na mitaani, hlamshauri za miji ziweke sehemu za kutupa taka kila mtaa na kila baada ya mita kadhaa. Wawepo watu wa kukusanya taka hizo pia. Hivyo, taka kama bidhaa izalishe ajira.
Utaratibu ukiwekwa ziwekwe na adhabu na zitekelezwe; mathalan, anayekamatwa akitupa takataka ovyo, alipishwe elfu 50 hapo hapo, kama hana, apewe fagio kufanya usafi kwa muda fulani utakaopangwa. Hivyo hivyo, kwa anayekutwa anajisaidia haja ndogo kichochoroni au kando ya barabara.
Mengi yanawezekana, tukiamua

No comments: