Rais Paul
Kagame wa Rwanda.Rwanda sasa itapiga kura ya maoni katika kipindi cha
wiki ijayo juu ya mabadiliko ya katiba kumruhusu Rais Paul Kagame
kuwania muhula wa tatu wa kuiongoza nchi hiyo, serikali ya nchi hiyo
imetoa tamko .
Kufuatia mabadiliko hayo ya kikatiba, kuna uwezekano wa rais Paul Kagame kusalia madarakani mpaka kufikia mwaka 2034.
Kwa
mujibu wa serikali, wanyarwanda waishio ughaibuni watapiga kura Disemba
17, na siku inayofuata ndio watapiga kura wanyarwanda waishio nchini
Rwanda.
Hata
hivyo, jaribio hilo limekwisha kulalamikiwa na nchi za umoja wa ulaya
ikiwemo Marekani ambayo imemtaka Rais Kagame kuwa mfano wa kuigwa katika
Ukanda wa Maziwa Makuu kwa kuachia madaraka mwishoni mwa utawala wake
ambao unafikia kikomo mwaka 2017.
Naye rais
Paul Kagame ameijibu kauli hiyo kwa kutaka mataifa mengine kuacha
kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Afrika Mashariki.
Baraza la
Senet nchini humo limeshatoa baraka zake kwa muswada huo wa mabadiliko
ya katiba mwezi uliopita na kumruhusu Kagame kugombea tena nafasi hiyo
mnamo mwaka 2017.
Wakati
mabadiliko mengine tarajiwa ya kufupisha muda wa utawala kwa miaka 7
hadi 5 na kuweka ukomo wa madaraka kwa vipindi viwili tofauti, sheria
hiyo haitakuwa na nguvu mpaka kufikia mwaka 2024, hapo tena Rais Paul
Kagame ataweza kugombea kwa awamu mbili tofauti za miaka 5.
Mabadiliko hayo yanatabiriwa kupitishwa bila upinzani wowote kwa kumpa rais Kagame kura ya ndio.
Chama cha
Paul Kagame cha Patriotic Front, kilikomesha mauaji ya kimbari
yaliyotokia nchini humo mnamo mwaka 1994 na kukitoa madarakani chama cha
Wahutu wenye msimamo mkali.
Katika mauaji hayo ya kimbari inakadiriwa kuwa wa Tutsi laki nane waliuawa.
Rais
Kagame mpaka sasa hajathibitisha kama atagombea tena nafasi hiyo mnamo
mwaka 2017 kama atapewa ridhaa, ingawa ameahidi kutoa maamuzi yake ya
endapo atagombea ama la baada ya kupigwa kwa kura ya maoni.


No comments:
Post a Comment