WATANZANIA
wametakiwa kutumia technolojia ya mawasiliano ikiwemo kufanya mikutano
kwa njia ya video ambayo itawaondolea gharama ya kusafiri na hivyo
kuokoa fedha na muda.
Rai
hiyo imetolea hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Charles
Senkondo wakati akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa
kazi wa video conference kati ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Taasisi zake, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za
mitaa.
Senkondo
alisema kufanya mikutano kwa njia ya video kunamfanya mtu asisafiri na
hivyo kuepukana na ajali, kutopoteza muda awapo safarini na na kupata
wasaa wa kukaa na familia yake.
“Kuanzishwa
kwa TaGLA kumeongeza uwezo wa kufanya kazi kwa ubunifu zaidi, kwa njia
ya kisasa, kwa maamuzi zaidi ya kiuendeshaji kwa kuangalia kila mara
mahitaji ya wadau na kutumia mbinu za soko katika utoaji wa huduma
bora”.
“Kabla
ya kukuwa kwa teknolojia watu walikuwa wanasafiri umbali mrefu kwenda
kushiriki mikutano hivi sasa wamepunguza safari zisizo na umuhimu. Mtu
atasafiri katika mikutano ya umuhimu tu zamani ilikuwa lazima mtu aje
sasa hivi anafuatwa popote alipo na kuletwa katika video conference”,
alisema Senkoro.
Akiongelea
kuhusu kituo hicho Mkurugenzi huyo alisema zaidi ya washiriki elfu 20
wameshiriki midaharo na mafunzo 783 ya kubadilishana maarifa kupitia
Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) .
Senkondo
alisema wakala hiyo imeweza kutoa mafunzo kwa viongozi wakiwemo
mawaziri, wakuu wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi na kuleta
urahisi wa vikundi na watu waliotengwa kijiografia kuonana, kusikilizana
na kukubaliana kwa wakati mmoja.
“Wakala
kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa
kutumia mitandao ya teknolojia imeweza kufundisha watendaji wakuu wa
Taasisi za Serikali, wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya zote na
wakurugenzi wa rasilimali watu wapatao 1,200 mfumo wa malipo ya
mishahara kwa watumishi wa Serikali (HCMIS) Lawson version 7”, alisema
Senkoro.
Mkurugenzi
huyo mtendaji alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni fikra
potofu juu ya matumizi ya TEHAMA na kukubalika kwa kasi kwa teknolojia
na kuwaomba waandishi wa habari pamoja na wadau wengine kuelimisha
wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya Tehama.
Senkoro
alisisitiza, “Tunawaalika wadau mbalimbali wakiwemo taasisi za Serikali
na zisizo za kiserikali, waandishi wa habari, watu binafsi na asasi za
jamii watumie huduma zetu ambazo tunazitoa kwa gharama naafuu kuweza
kuwafikia wadau wengi kwa muda mfupi bila kujali umbali au changamoto za
kijiografia.
Wakala
wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao umewezesha kufanyika kwa mahakama kwa
kutumia mikutano ya video katika kesi mbalimbali kwa kutoa ushahidi wake
kwa njia ya video na kusaidia kupunguza gharama na kuhamasisha maamuzi
na hivyo utoaji wa haki katika kesi husika.
Mkutano
huo wa kazi wa video conference kati ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Taasisi zake, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za
Serikali za mitaa ulijumuisha viongozi wa Serikali kutoka mikoa ya
Dodoma, Lindi, Geita, Singida, Pwani, Mara, Iringa, Mtwara, Shinyanga na
Njombe.
No comments:
Post a Comment