Tajikistan ni moja ya nchi ambazo ziko
bara la Asia, kilichoteka vichwa vya habari sasahivi ni ishu ya
‘MARUFUKU’ iliyopigwa kuhusiana na shamrashamra za sikukuu za Christmas
siku chache zijazo.
Tangazo limetolewa kwamba ni marufuku
kabisa kwenye maeneo ya shule na vyuoni kupiga fataki, marufuku kuweka
mapambo ya miti pamoja na shamrashamra za zawadi na mambo mengine ambayo
kwa kawaida huwa yanafanyika kwenye sherehe.
Hii sio mara ya kwanza kutolewa tangazo la aina hiyo, mwaka 2014 ilipigwa marufuku kuingizwa sanamu za ‘Father Christmas‘ zilizotengenezwa Russia… na pia mwaka 2013 na 2014 iliwahi kutokea kesi za watu kukamatwa kwa kosa la kuvaa nguo kama mazombi baada ya Serikali kupiga marufuku sherehe za Halloween
No comments:
Post a Comment