''Wanawake wa Kiislamu walivua hijab na kuwastiri wanawake wakristu ilikuwaokoa wasiuawe.'' Muasiriwa
Mwalimu
mmoja aliyenusurika kifo katika shambulizi la basi lililotekelezwa na
wapiganaji wa Al shabaab hapo jana ameiambia BBC kuwa wanawake wa
Kiislamu walivua hijab na kuwastiri wanawake wakristu ilikuwaokoa
wasiuawe.
Mwalimu
huyo ambaye ni mmoja wa abiria wa basi hilo la umma waliojeruhiwa wakati
wa shambulizi hilo la alfajiri anasema punde baada ya basi hilo
kutekwa, Magaidi hao waliwaeleza kuwa waislamu wote wako salama.
''Walituambia kuwa sisi waislamu tulikuwa salama na hivyo tukang'amua kuwa wanawalenga wakristu''
''Hapo ndipo wanawake wakavua hijab zao na kuwastiri wanawake wakristo''.
''Kwa
sababu walikuwa ni wanaume ,wanawake walijitenga na kuwaficha wanawake
wakristo na hivyo kuwaokoa wasiuawe'' alisema mwalimu huyo ambaye
anauguza majeraha mjini Mandera.
Al shabaab:Waislamu waliwafunika Hijab wakristo''Ilikuwa vigumu kutambua nani ni muislamu na nani siye''
Hapo jana, Wapiganaji wa Alshabaab waliteka basi moja la usafiri wa umma na kuua watu wawili.
Idadi ya
wahasiri ilikuwa ndogo kufuatia jitihada za abiria waislamu kuwaficha na
kuwaokoa wenzao wakristo waliokuwa wakisafiri pamoja.
Tukio hilo limevutia hisia kali kote duniani.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa Waislamu.
Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.
No comments:
Post a Comment