Mtoto katika kitongoni kimoja cha mji wa Syria wa Al-Hol, Novemba 19, 2015.
Na RFI
Watu
wasiopungua 26 wameuawa Jumatatu hii kaskazini mwa Syria katika
mashambulizi ya anga yanayokisiwa kutekelezwa na muungano wa kimataifa
unaoongozwa na Marekani, shirika la Haki za Binadamu (OSDH) limetangaza.
atoto
saba na wanawake wanne ni miongoni mwa watu waliouawa katika
mashambulizi hayo yaliolenga kijiji cha Al-Hol, ambacho mwezi uliopita
kiliondolewa mikononi mwa kundi la Islamic State (IS) na waasi wa
Kiarabu na wa Kurdi, shirika la haki za binadamu limeeleza.
Mapema
Jumatatu wiki hii serikali ya Syria imeunyooshea kidole cha lawama
muungano wa kimataifa kuendesha mashambulizi kwa mara ya kwanza katika
kambi ya jeshi kuuawa wanajeshi kadhaa, madai ambayo yamekanushwa na
muungano unaoongozwa na Marekani, ambao umethibitisha kuwa mashambulizi
yake yamelenga kundi la Islamic State (IS).
Damascus
imejibu kwa nguvu baada ya vifo vya askari wake watatu waliouawa siku ya
Jumapili katika mashambulizi ya angani katika kambi ya jeshi ya Deir
Ezzor, mashariki mwa Syria.
Damascus
imeushtumu moja kwa moja "muungano unaoongozwa na Marekani" kwa"uchokozi
wa wazi" ambao "unakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa."
"Tunatoa
wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua muhimu ili
kuzuia tukio kama hili lisirudi si kutokea", wizara ya mambo ya nje
imeongeza katika barua iliyomtumia Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na
Baraza la Usalama la Umoja huo.
Alhamisi
Desemba 4, Uingereza iliendesha mashambulizi yake ya kwanza ya anga
nchini Syria dhidi ya ngome za kundi la Islamic State, masaa kadhaa tu
baada ya kupewa idhni na Bunge.
Rais wa
Marekani Barack Obama, ambaye anaongoza muungano wa washirika nchini
Syria dhid ya IS, alikaribisha uamzi huo, akisema kwamba Marekani imekua
ikisubiri jeshi la anga la Uingereza kujiunga katika shughuli za
kijeshi nchini Syria.


No comments:
Post a Comment