Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Efm radio
kwa kushirikiana na Benki ya DTB pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya
Kinondoni chini ya mkuu wa wilaya hiyo, Paul Makonda wameamua kuunga
mkono na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dk. John Pombe Magufuli la kuadhimisha siku ya Uhuru Desemba 9, mwaka
huu kwa kufanya usafi wa mazingira.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuondoa ama kumaliza kabisa tatizo la magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Akizungumza
jana katika ofisi za Efm zilizopo Kawe jijini Dar, Meneja Mawasiliano
na Mahusiano wa Radio hiyo, Denis Ssebo amesema siku hiyo wameipa kauli
mbiu ya “Naona aibu kuishi na uchafu” wakiunga mkono kauli mbiu ya
Wilaya ya Kinondoni inayosema “Usafi uanze na mimi”.
Maeneo
wanayotarajia kuyafanyia usafi ni barabara inayoanzia Morocco kuelekea
Magomeni, kuanzia saa 2 asubuhi na kuendelea, hivyo amewaomba kutumia
nafasi hiyo kuwaomba wateja wa Benki ya DTB na wasikilizaji wa Efm
pamoja na wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza siku hiyo ya Uhuru
kwa usafi wa mazingira ya nchi.


No comments:
Post a Comment