Ndege
iliyozinduliwa na Shirika la Ndege la Etihad ilipowasili katika uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam na kupokelewa na magari
ya zimamoto kwa kumwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege
za shirika la ndege la Etihad lenye makao makuu Abudhabi. Uzinduzi huo
unatoa fursa sasa kwa watanzania kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es
salaam mpaka Abudhabi kila siku.
Makamu
wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad Bw. Daniel
Barranger akisalimiana na Balozi wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini
Tanzania Mh. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi mara baada ya uzinduzi rasmi wa
shirika hilo uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijiji Dar es salaam. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa
watanzania kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi.
Makamu
wa Rais- Mauzo Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad Bw. Daniel
Barranger (kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya uzinduzi wa shirika la ndege la Etihad ambao
ulifanyika siku ya jana jijini Dar es salaam.Pamoja nae ni Mh. Balozi wa
Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdullah Ibrahim Al
Suwaidi.
Mh.
Balozi wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdullah
Ibrahim Al Suwaidi akitoa hotuba yake kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya uzinduzi rasmi wa shirika la ndege la Etihad
uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijiji
Dar es salaam.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakifuatilia mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mara
baada ya uzinduzi rasmi wa shirika la ndege la Etihad hapa nchini.
Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania kusafiri moja kwa moja
kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.
Shirika la
ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za Kiarabu, leo hii
imeendelea kuimarisha uwepo wake Afrika Mashariki kwa kuzindua huduma
zake mpya za safari za ndege baina ya Dar es Salaam, mji mkubwa zaidi
nchini Tanzania na Abu Dhabi, mji mkuu wa Falme za kiarabu (UAE).
Mara baada
ya ndege inayozinduliwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere, ililakiwa na mizinga ya maji kama ishara ya heshima
kubwa na abiria walioshuka wakikaribishwa kwa burudani ya ngoma za
kitamaduni za Tanzania.
Shughuli ya kukata utepe ilifuatia ambayo katika kuweka kumbukumbu ya tukio hilo la kufana ambapo lilifanikishwa na
– Dr Shaaban Mwinjaka, Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi
– Dr Adelhelm James Meru, Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Maliasili
– H.E. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania Nchi za Falme za kiarabu
– H.E. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, Balozi wa Nchi za Falme za kiarabu Tanzania
– Daniel Barranger, Makamu wa Rais wa Mauzo ya kimataifa wa shirika la ndege la Etihad
– Mhandisi:Thomas Haule Mkurugenzi Mamlaka ya Ndege
Dar es
Salaam imekuwa ni kituo cha tatu kwa shirika la ndege la Etihad Afrika
Mashariki, baada ya Nairobi na Entebbe,na ya tisa barani Afrika.
Huduma hii
mpya ikiwa inaendeshwa na ndege aina ya Airbus A320 yenye madaraja
mawili, siti 16 daraja la “Business” na siti 120 daraja la “Economy”
ikiwa imelenga wafanya biashara na wanaosafiri kwa starehe moja kwa moja
kila siku baina ya Dar es salaam na Abu Dhabi, pamoja na uunganishaji
mrahisi kwenda nchi nyingine ukanda wa GCC, Ulaya, India, Asia
kaskazini, Asia ya Kusini na Australia.
Bw.
Barranger, alisema “uzinduzi huu wa safari za shirika la ndege la Etihad
kuja Dar es Salaam zimewiana na mkakati wetu wa kulenga masoko yanayo
endelea kukua kwa kasi”.
“Dar es
Salaam ni mji ambao umekuwa kivutio sana kwa watalii wanaotaka kufahamu
tamaduni na historia ya Tanzania, pia ni mlango wa vivutio vya kitalii
vingi vya kitaifa na kimataifa ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za
wanyama kama Serengeti na kisiwa cha Zanzibar.
“Nchi Falme
za kiarabu ni mdau mkubwa wa kibiashara na Tanzania, huduma hii mpya
itaongeza nguvu ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili.
Ratiba za safari za ndege zitawapa wageni urahisi wa kupata ndege za
kuunganisha safari kwenda nchi nyingine, ikiwa inahudumia safari nyingi
sana baina ya Tanzania na nchi nyingi katika mtandao wetu wa kimataifa
kama Ahmedabad na Mumbai nchini India au Beijing na Shanghai nchini
China.”
“Pamoja na
kutoa huduma ya moja kwa moja kwa watalii na wafanya biashara baina ya
nchi hizi mbili, safari hizi pia zimeendelea kuimarisha uwepo wetu
Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla” aliongezea.
Shirika la
ndege la Etihad limekuwa likiongeza uwepo wake barani Afrika tokea
walipozindua safari zake za kwanza barani Afrika, huko Cairo November
2004. Baada ya hapo zikafuatia Casablanca, Entebbe, Johannesburg,
Khartoum, Lagos, Nairobi, (15 January 2015) na Mahe huko visiwa vya
shelisheli na mipango ya uzinduzi katika mji wa Rabat, Morocco katikati
ya mwezi Januari 2016.
Ratiba za shirika la ndege la Etihad, Dar es Salaam kuanzia tarehe 1 December 2015:
Flight No. | Kutoka | Kuondoka | Kwenda | Kufika | Idadi | Ndege |
EY681 | Abu Dhabi (AUH) | 8:20 | Dar es Salaam (DAR) | 13:00 | Kila Siku | A320 |
EY682 | Dar es Salaam (DAR) | 13:50 | Abu Dhabi (AUH) | 20:15 | Kila Siku | A320 |
Zingatia: Muda wa kuondoka ni majira ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment