Serikali Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Namna Ya Kuadhimisha Siku Ya Uhuru - LEKULE

Breaking

9 Dec 2015

Serikali Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Namna Ya Kuadhimisha Siku Ya Uhuru


Serikali imetoaufafanuzi kuhusu namnaya kuadhimisha siku yaUhuru yaani Tarehe 9 Desemba, 2015 kuwa siku hiyo sio siku ya mapumziko.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Omben iSefue, amesema siku hiyo ni siku ya kazi kam ailivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Mamlaka aliyonayo kisheria.

Katika Ufafanuzihuo,Balozi Sefue amesema endapo wafanyakazi watakuwa na kazi muhimu za kufanya katika ofisi zao wanaweza kwenda kazini kama kawaida,vinginevyo washiriki kufanya usafi katika maeneo wanayoishi au maeneo ya nayozunguka sehemuzao za kazi.

Aidha,amesisitiza kuwa kampeni ya usafi itafanywa nchi nzima na kuwa sihi viongozi katika mamlaka za serikali za mitaa kulisimamia zoezi hilo kikamilifu.

GersonMsigwa
KaimuMkurugenziwaMawasiliano, IKULU

08 Desemba, 2015

No comments: