REAL MADRID YAKUTANA NA MAKALI YA SHERIA,YATUPWA NJE KOMBE LA MFALME - LEKULE

Breaking

5 Dec 2015

REAL MADRID YAKUTANA NA MAKALI YA SHERIA,YATUPWA NJE KOMBE LA MFALME

Denis Cheryshev kulia akipiga shuti lililoipatia Real Madrid goli la kuongoza

Real Madrid imeondoshwa kwenye michuano ya Copa del Rey baada ya kumchezesha mchezaji anayetumikia adhabu ya kutocheza mechi moja,tukioa hilo lilitokea dhidi ya timu ya Cadiz siku ya Jumatano wakati mchezaji huyo Denis Cheryshev raia wa Urusi aliweza kufungua akaunti ya magoli ya Real Madrid katika ushindi wao wa magoli 3-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya mchezo huo.
Mchezaji huyo wa eneo la ushambuliaji akitokea pembeni alitakiwa kutoshiriki mchezo huo baada ya kupewa adhabu hiyo wakati akicheza timu ya Villarreal kwa mkopo,lakini maafisa wa Real Madrid ambao walimrudisha kwenye kikosi hicho kutoka kwenye huduma yake ya awali ya kucheza kwa mkopo wamenukuliwa wakisema hawakuelezwa juu ya adhabu hiyo.

Denis Cheryshev alitolewa mapema kwenye kipindi cha pili baada ya mapumziko baada ya Real Madrid kugundua makosa yao,hali hiyo haikuifanya kamati ya mashindano hayo kushindwa kuitupa nje ya michuano hiyo miamba halisi ya soka la Hispania Real Mdarid na huku wakiipiga faini ya Euro 6001 na kuwatupa rasmi nje ya michuano hiyo kwa kosa hilo la kumchezesha mchezaji asiyeruhusiwa kisheria.

No comments: