Rais Magufuli amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Dkt. Philip Mpango kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na mamlaka hiyo ambayo imeongeza ukusanyaji wa Mapato na kwa mara ya kwanza mwezi huu ukusanyaji wa mapato hayo unatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300
Kutokana
na mafanikio hayo amewahakikishia watanzania kuwa fedha kwa ajili ya
kutimiza ahadi ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari
ambazo ni kiasi cha shilingi Bilioni 131 zitatengwa mwezi huu na
kupelekwa moja kwa moja katika shule husika.
Amesema
wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa
watapatiwa nakala za taarifa za ugawaji wa fedha hizo na kuonya kuwa
hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzitumia vibaya.
Dkt.
Magufuli ameongeza kuwa fedha hizo ambazo ni pamoja na fedha za
maendeleo, fedha za mitihani na fedha vifaa vya kufundishia zitaanza
kutumwa kila mwezi kuanzia mwezi huu wa kumi na mbili.
Msikilize Hapo Chini Akiongea
Msikilize Hapo Chini Akiongea
No comments:
Post a Comment