JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA
BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za
rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius
Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga (OSB) kilichotokea
Ijumaa tarehe 18 Desemba, 2015 katika hospitali ya Mtakatifu Joseph Peramiho,
Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mhashamu
Askofu Nkalanga aliyekua Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba alistaafu uaskofu
mwaka 1974 na kujiunga na watawa wabenediktini wamonaki ambapo aliamua kwenda
kuishi katika Abasia ya Hanga iliyopo katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Katika
salamu zake Rais Magufuli amesema Askofu
Nkalanga aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96 atakumbukwa kwa mchango
wake mkubwa alioutoa kuhimiza imani na uchapakazi kazi katika kipindi chote cha
miaka 54 ya uaskofu wake na utawa wake akiwa katika Abasia ya Hanga.
Amesema
Marehemu Askofu Nkalanga ambaye baada ya kustaafu aliamua kuingia katika utawa
akianzia katika ngazi ya chini kabisa ya Unovisi
hadi alipofunga nadhili za milele za utawa mwaka 2009, ameacha mfano mzuri
unaohimiza jamii kuishi kwa upendo, unyenyekevu na kutokata tamaa.
"Kupitia
kwako Baba Askofu Ngalalekumtwa napenda kuwapa pole nyingi Askofu Mkuu wa Jimbo
Kuu Katoliki la Songea, Abate wa Abasia ya Hanga, watawa na waumini wote wa
kanisa Katoliki kwa kupoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika
maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla" amesema Rais Magufuli.
Rais
John Pombe Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu Mhashamu
Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga mahali pema peponi, Amina.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
20
Desemba, 2015
No comments:
Post a Comment