Na RFI
Rais wa
Marekani Barack Obama amesema Alhamisi hii kuwa sababu za wahusika wa
shambulizi lililogharimu maisha ya watu wengi katika kaunti ya San
Bernardino (California) Jumatano usiku wiki hii zilikua bado
hazijajulikana, akisema kwamba kuna uwezekano kuwa shambulizi hio
lilikua la kigaidi.
"Katika
hatua hii hatujajua ni kwa nini tukio hili la kutisha liilitokea", Obama
amesema kutoka Ikulu ya White House ambapo lilikuwepo baraza la kitaifa
la usalama.
"Tunajua
kwamba watu wawili ambao waliuawa walikuwa walijihami kwa silaha na
inaonekana kuwa walikua na silaha nyingine katika nyumba zao", Rais
Obama ameonge."Lakini hatujui ni kwa nini walifanya hivyo, hatujui nia
yao."
"Inawezekana
kwamba shambulizi hili linahusiana na ugaidi, lakini hatujui.
Inawezekana pia kwamba shambulizi hili linahusiana na mahali pa kazi",
aliendelea Rais Obama, akiongeza kuwa FBI ilikuwa imeanzisha uchunguzi.
Shambulizi
hili, ambalo liligharimu maisha ya watu wasiopungua 14, lilifanywa na
watu wawili ambao walikua walijihami kwa silaha kubwa, ambao waliuawa na
polisi muda mchache baadae.
No comments:
Post a Comment