Je, UMETOZWA NAULI KUBWA KWENYE BASI KULIKO UMBALI UNAOKWENDA?
Fanya yafuatayo:
1. Bishia nauli uliyotozwa kuwa si halali. mfano kama unakokwenda ni Dar-Mafinga, nauli inapaswa kuwa 20,000 wewe ukatozwa Dar - Njombe 25,000, bishia. Kondakta akikataa lipa, ingia kwenye gari.
2. Atakupa tiketi imeandikwa Dar - Mafinga 25,000 au atakupa tiketi imeandikwa Dar-Njombe 30,000. Pokea
3.
Ipige picha hiyo tiketi, au iscan kisha itume kwenda nambari 0682
887722(kwa whatsapp, telegram au wechat) ukielezea kuwa umetozwa nauli
kubwa kuliko umbali wa safari au umepandishwa bus ordinary wakati wewe
ulitozwa nauli ya luxury. Na kwamba kondakta amekataa kukuandikia tiketi
ya unakokwenda badala yake akakuandikia tiketi inayoonesha kituo
ambacho basi linaishia. Au Tuma ujumbe au piga simu kwenda 0800 110 019
au 0800 110 020 (bure). Namba hizi tumia hata pale gari inapokatisha
ruti au kuwatelekeza njiani baada ya kuharibika.
4.
Basi litasimamishwa kituo cha mbele, utarudishiwa nauli yako. Kama
limekamatwa na askari polisi basi dereva au kondakta atarudisha nauli na
30,000 itamhusu. Akikamatwa na SUMATRA basi atarudisha nauli na faini
ya sh.250,000 itamhusu.
SAMBAZA UJUMBE HUU KADIRI UWEZAVYO, MUELIMISHE MWENZIO
Imetolewa na
RSA TANZANIAUSALAMA BARABARANI JUKUMU LETU SOTE
No comments:
Post a Comment