Serikali
imetoa tamko kwa vyombo vyote vya habari nchini kuanzia january mosi
mwakani kutotumia miziki ya aina yeyote ,wa ndani au nje bila kibali
kutoka Cosota.
Wakitoa
tamko hilo kwa pamoja waziri wa habari michezo na utamaduni Nape Nnauye
na waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage wamewataka wamiliki wa
vyombo vya habari kutoa ushirikiano.
Nape
amesema atalisimamia zoezi hilo na kutoa tahadhari kwa chombo chochote
cha habari kitachokiuka tamko hilo hatakionea haya kukifungia leseni.
Naye
waziri wa viwanda na biashara amesema kuna kampuni ya wazawa ya CMEA
ambayo imeanza kazi ya kusimika mitambo yake kila mkoa itakayofanya
kazi ya kunakili kila kinachofanyika kwenye kila chombo cha habari.
Kwa
upande wa wasanii msanii Nick wa pili amependekeza muziki wa wasanii wa
nje ya tanzania uchajiwe gharama kubwa ili muziki wa Tanzania upate
nafasi kubwa.
No comments:
Post a Comment