Mwanasoka Alfred Pacheco apigwa risasi na kufariki. - LEKULE

Breaking

29 Dec 2015

Mwanasoka Alfred Pacheco apigwa risasi na kufariki.



Ikiwa ni zaidi ya wiki moja toka mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta itangazwa kauwawa kwa risasi, December 28 mitandao mingi ya Ulaya imeripoti kifo cha staa mwingine wa soka aliyeuwawa kwa kupigwa risasi. December 27 aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya El Salvador Alfred Pacheco ameuawa kwa kupigwa na risasi wakati akiwa katika kituo cha mafuta cha mji wa Santa Ana.
28pacheco
 Alfred Pacheco ambaye alikuwa anamudu kucheza nafasi ya beki wa kushoto alipigwa risasi na watu wengine wawili wakijeruhiwa katika shambulio hilo ambalo maafisa usalama bado wanachunguza tatizo ilikuwa lipi.  Alfred Pacheco amecheza muda mrefu zaidi kwenye timu yake ya taifa na amewahi kuchezea vilabu tofauti tofauti ikiwemo New York Red Bulls ya Marekani.
3036523707_6abffe066c (1) (1)
Tukio hili linakuja ikiwa ni wiki kadhaa zimepita toka auwawe kwa kupigwa risasi mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Peralta akiwa mapumziko nyumbani kwao Honduras. Kama utakuwa unakumbuka vizuri  Pacheco alifungiwa maisha kucheza soka kutokana na kashfa ya kupanga matokeo mwaka 2010-2013 pamoja na wachezaji wengine 13.

No comments: