Mheshimiwa Zitto pia alikuwapo
Chupa ya Hennessy 250 Collectors blend iliyotengenezwa maalum kusherekea miaka 250 ya kinywaji hicho.
Kwa ndani kulikuwa na eneo lilikowekwa picha mbalimbali kuhusiana na historia ya kinywaji hicho
Wageni waliojumuika pamoja siku hiyo
MWANAMUZIKI
mahiri wa muziki wa Hip Hop nchini, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana
Fa amezikonga nyoyo za mashabiki wake kwenye hafla ya kuadhimisha miaka
250 ya kinywaji cha Hennessy yaliyofanyika katika baa ya Oasis Masaki.
Mwana
Fa alianza kuimba majira ya saa nne ambapo alianza kwa kuimba nyimbo
zake mbalimbali zilizowahi kutamba kama vile, Mimi na Mabinti pamoja na
nyinginezo za zamani.
Baada ya kumaliza nyimbo hizo za miaka ya nyuma akaanza kuimba nyimbo zake za sasa ukiwamo ule wa Mfalme na nyinginezo mpya.
Watu
wengi walihudhuria hafla hiyo ya maadhimisho ya kinywaji hicho iliyoenda
sambamba na maonesho ya michoro mbalimbali kuhusianana historia ya
kinywjai hicho ambacho asili yake ni Ufaransa.
Pia watoa burudani mbalimbali kama vile kundi la Mosaic Collective pamoja na Mac Band walitoa burudani.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo,
mratibu wa maadhimisho hayo ambae pia ni mmiliki wa baa ya Oasis Nuru
Mosha alisema kuwa kinywaji hicho kimekuwa karibu zaidi na sanaa ya
Tanzania kwa ujumla mbali na kufanya biashara.
Mosha
alisema kuwa kwa kuwa mwanzilishi wa kinywaji hicho alikuwa ni mtu
mpenda sanaa hasa aiwa anajishughulisha na sanaa ya uchoraji na hivyo
wageni wanaotembelea michoro hiyo wanapata kufahamu kiundani zaidi
historia ya kinywaji pia.
No comments:
Post a Comment