Kocha
wa Manchester United, Louis Van Gaal (pichani) ambaye kibarua chake
kipo katika kipindi kigumu kufuatia kipigo cha goli 2 kwa bila kutoka
kwa Stoke City amesema anafikiri anatakiwa kuacha kibarua cha kuinoa
klabu hiyo.
Akiwa
katika wakati mgumu wa hatma ya kibarua chake Van Gaal ameshudia timu
yake ikifungwa goli 2 kwa bila na kuwa mchezo wa 7 kufungwa kwa msimu
huu na kikiwa kipigo cha kwanza ndani ya miaka 54 Manchester United
kufungwa siku ya Boxing Day huku ikiwa ipo nje ya timu nne za juu kwa
Ligi Kuu ya Wingereza na kuwa imetolewa katika hatua ya makundi ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya UEFA.
Alipolizwa na kituo cha Sky Sports baada
ya mchezo wa Manchester United na Stoke City kama uongozi wa Manchester
United bado unampa ushirikiano Van Gaal alijibu “Ninaweza kuwa kimya
mimi binafsi, hilo ni jambo ambalo nazungumza na Ed Woodward [mtendaji
mkuu] kuhusu yeye na sio wewe [mwandishi],
“Sio
lazima mpaka klabu inifukuze mimi, muda mwingine ninafanya maamuzi
mwenyewe ya kuondoka, ninahitaji kwanza kuzungumza na bodi ya Manchester
United na wafanyakazi wenzangu na hata wachezaji ila sio wewe”
Pia
Van Gaal akalizwa kama ataendelea kuifundisha timu hiyo “Ni ngumu
kwasababu nimekuwa sehemu ya kupoteza michezo minne, tumepoteza na watu
wananiangalia mimi … natakiwa kushughulikia hilo lakini muhimu zaidi ni
wachezaji kushughulikia sababu wao ndiyo wanaocheza na sasa ni jambo
kubwa. Najaribu kufanya kila kitu lakini hali hii imeshakuwa kubwa na
kubwa kila mchezo na tunatakiwa kushughulikia hilo”
No comments:
Post a Comment