Meek Mill matatani, licha ya Nicki Minaj kumtetea Mahakama haijamuacha bure! - LEKULE

Breaking

18 Dec 2015

Meek Mill matatani, licha ya Nicki Minaj kumtetea Mahakama haijamuacha bure!

Mwaka huu wa 2015 hautoisha poa kwa rapper wa Maybach Music Group, Meek Millkwani baada ya kusimama Mahakamani kwa zaidi ya wiki mbili inaonekana jitihada zake za kujitetea kwanini hajatii sheria za kifungo chake cha nje hazijairidhisha Mahakama ya Philadelphia.
jela2
Meek Mill & Nicki Minaj.
Jana rapper huyo alipanda kizimbani kujitetea kwa mara ya mwisho lakini baada ya saa moja ya kujaribu kuishawishi Mahakama, mambo yanaonekana si shwari kwa Meek Milllicha ya mpenzi wake piaNicki Minaj kusimama Mahakamani na kumtetea.
>>> “Mimi sio gangsta, Mimi sio mualifu, sasa hivi nina malkia wangu Nicki Minaj. Nakubali sipo perfect lakini najaribu kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yangu na yake. Naamini naweza kuwa rapper bora kwa karne hii. Nimebadilika, mimi sio yule wa miaka ya nyuma…” <<< Meek Mill alijitetea mbele ya Mahakama.
jela3
Chris Brown.
Mahakama ya Philadelphia imesema hukumu ya Meek Mill itatolewa tarehe 5 February 2016… baadhi ya mastaa kama Chris Brown wamejitokeza kutoa support yao kwa Meek Mill kwenye hizi tweets zake tano nilizofanikiwa kuzinasa kupitia page yake ya Twitter@ChrisBrown.
jail1
>>> “Natamani jaji angeona ushawishi alionao Meek Mill nje ya jela kuliko ndani yake. Mnataka kumfunga lakini vipi kuhusu FREDDIE GRAY?” <<< @ChrisBrown.
jail2
>>> “System yetu imevurugwa. DA’s na MAJAJI wanavurugwa kama watu wengine wote na wanavuruga maisha ya watu!” <<< @Chris Brown.
jail3
>>> “Sipo kwenye kifungo chochote cha nje kwahiyo nina uwezo wa kuwaambia kiss my a***!“<<< @ChrisBrown.
jail4
>>> “Mnafikiri watu wataendelea kukaa na kutazama ujinga huu ukiendelea? Mnataka kuziondoka bundiki mtaani ili mzipe nguvu Sheria za Kijeshi” <<< @ChrisBrown.
jail5
>>> “Ndio, Nimesema!” <<< @ChrisBrown.
Meek Mill amekuwa akitumikia kifungo cha nje toka mwaka 2009 ambapo alikutwa akimiliki na kutumia bunduki kinyume na Sheria za Marekani pamoja na kutumia dawa za kulevya. Alifungwa kwa miezi 11 hadi 23, badaaye akatolewa na kupewa kifungo cha nje lakini mwaka jana alivunja sheria za kifungo hicho na kukaa jela kwa miezi 6.

No comments: