Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mtandao wa Face book.
Mtuhumiwa
huyo aliyefahamika kwa jina la Carolne Kajela, alikamatwa jioni ya
desemba 12, mwaka huu eneo la Uyole Jijini hapa, baada ya kuandika
katika ukurasa wake wa Facebook kupitia kundi la Kwinyara Let’s talk
kuwa, mmiliki wa mabasi ya Rungwe Express anaingiza mabasi hayo kupitia
taasisi ya dini.
“Mtumbua
majipu atumbue na hili.. mmiliki wa mabasi ya RUNGWE EXPRESS anapitisha
mabasi kupitia taasisi moja ya kidin imbombo... jilipo,” unasomeka ujumbe huo, ambao mpaka anakamatwa ulikuwa umependwa na watu 35 na kuchangiwa maoni na watu 120
Taarifa
kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema baada ya mtuhumiwa huyo
kukamatwa na kuhojiwa, amekiri kosa na kuomba asamehewe kwani shetani
alimzidi.
Mmiliki
wa mabasi hayo Yohana Sonelo, alipohojiwa amekiri kampuni yake kupeleka
mashitaka polisi na kwamba wanahitaji athibitishe alichokiandika
mtandaoni, lasivyo sheria ya makosa ya mtandao namba 14 ya mwaka 2015
ambayo ilianza kutumika Septemba Mosi mwaka huu ifuate mkondo wake.
Kamanda
wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kumkamata mtuhumiwa
huyo na kwamba taratibu za upelelezi zinaendelea kisha watapeleka
jalada kwa mwanasheria wa serikali ili mtuhumiwa afunguliwe mashitaka na
afikishwe mahakamani.
No comments:
Post a Comment