Serikali
ya Marekani kupitia Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imetangaza
kusitisha msaada wa dola Milioni 472.8 ambazo ni sawa na takribani
shilingi trillion moja, kutokana na uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya
uchaguzi wa Zanzibar pamoja na mwenendo wa zoezi la ukamataji unaotokana
na sheria za makosa ya mtandao wakati wa uchaguzi.
Fedha hizo za zilikuwa zimelenga katika kusaidia sekta ya nishati na madini ikiwa ni pamoja na kuunganisha vijijini.
Balozi Mark B. Childress ametoa taarifa hii rasmi kwa serikali ya Tanzania
Fedha hizo za zilikuwa zimelenga katika kusaidia sekta ya nishati na madini ikiwa ni pamoja na kuunganisha vijijini.
Balozi Mark B. Childress ametoa taarifa hii rasmi kwa serikali ya Tanzania
*********
Tarehe
16 Disemba, Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) haikuichagua
Tanzania kwa mkataba wa pili. Bodi iliahirisha kupigia kura mkataba wa
pili, ikisubiri kutatuliwa kwa masuala ya kiutawala.
Bodi
inaweza kuangalia upya ustahilifu wa Tanzania mwaka 2016. Ninatumaini
kwamba Serikali ya Tanzania itachukua hatua hivi karibuni zitakazotatua
masuala hayo ya kiutawala. Halafu, Bodi itaweza kupiga kura kuichagua
tena Tanzania na kuidhinisha maendeleo ya mkataba.
Masuala
ya kiutawala ya Bodi yanaakisi maadili ya muda mrefu ya MCC. Kufutwa
kwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar kulisitisha mchakato wa
uchaguzi uliokuwa unaenda vizuri na kwa amani.
Matumizi
ya Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 kuwakamata watu waliokuwa
na kibali halali kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi yalikwaza uhuru wa
msingi wa kujieleza na kukutana.
MCC
imetiwa moyo na hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na Rais Magufuli za
kuimarisha vita dhidi ya ubadhilifu na rushwa. MCC inatumaini kuwa
jitihada hizo zitaendelea na kuleta mabadiliko ya kimfumo.
No comments:
Post a Comment