Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya akifungua semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha
watumiaji wa Huduma za Mawasiliano iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la
Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) katika ukumbi wa Mkapa
jijini Mbeya Desemba 15 -2015 ).
Picha Emanuel Madafa
Mwenyekiti Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano
(TCRA-CCC)Ndugu Stanley Mwabulambo (kulia) pamoja na Meneja wa
Mawasiliano TCRA Kanda ya Nyanda za juu kusini Mhandisi Lilian Mwangoka
wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika
ufunguzi wa semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za
Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 katika ukumbi wa Mkapa jijini
Mbeya.
Wananchi na baadhi ya watumishi wa serikali na mashirika binafsi
wakisikiliza kwa Makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas
Kandoro katika semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa
huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi
wa Mkapa jijini Mbeya.
Watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya wakifatilia kwa makini hotuba ya mkuu wa mkoa wa mbeya Abbasi Kandoro.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Mariam Mtunguja akizungumza
katika semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha watumiaji wa wa huduma za
Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 Mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa
jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za
Mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo akitoa neo katika semina hiyo ya
kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa Huduma za mawasiliano Mkoa Mbeya
Desemba 15-2015 katika ukumbi wa Mkapa jijini mbeya.
Wadau wakifuatilia mkutano
Kaimu Katibu mtendaji Baraza la Ushauri watumiaji wa Huduma za
Mawasiliano TCRA-CCC Ndugu Mary Msuya akiwasilisha maada kwa wanasemina
juu ya haki na wajibu wa Mtumiaji wa huduma za Mawasilino katika semina
hiyo yenye lengo la kuelimisha na kuhamsisha watumiaji wa huduma hizo
Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya.
Mhandisi toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Nyanda za
juu kusini Mbeya ( TCRA( Asajile Mwakisisile akitoa maada katika semina
hiyo.
Mmoja wa washiriki katika semina hiyo akichangia katika semina .
Mjumbe wa Baraza la Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) Ndgugu Nyanda
Shuli akitoa Maada juu ya Muundo ,Kazi na Majukumu ya Baraza la
watumiaji wa Huduma za Mawasiliano katika semina ya kuelimisha na
kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15
mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.
Washiriki wa semina hiyo ya Uhamasishaji na uelimisha wa huduma za Mawasilino wakifuatilia kwa Makini semina hiyo.
Picha ya pamoja na Meza Kuu.
Na EmanuelMadafa,Mbeya(jamiimojablogu )
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameyaasa Makampuni ya huduma za
Mawasiliano ya Simu Nchini kuhakikisha yanaboresha huduma zao kwa
kuhakikisha yanaondoa kero zote anazo kutana nazo mtumiaji wa mawasilino
hayo.
Amesema moja ya changamoto inayowakwaza watumaiji wa mawasilino
hayo ni pamoja na kuweka matangazo ya simu (Miito ya simu)ambapo hukatwa
kiasi cha pesa pasipo makubalino.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ametoa kauli hiyo
jijini Mbeya wakati akifungua semina ya kuelimisha na kuhamasisha
watumiaji wa huduma za mawasiliano iliyondesha na Baraza la Ushauri la
watumiaji wa huduma za mawasilino TCRA-CCC katika ukumbi wa Mkapa jijini
humo.
Amesema pamoja na kutambua mchango wa makampuni yanayotoa huduma
hizo za mawasiliano katika kuleta maendeleo ,nivyema makampuni hayo
yakahakikisha yanatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu unaonekana na
thamani inayolipwa na watumiaji wa huduma hizo sanjali na kutimiza
majukumu yao kwa watumiaji kama yalivyo ainishwa katika sheria na kanuni
za leseni.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amewataka watumiaji huduma hizo
za mawasiliano ya simu kujikita katika matumizi bora ya mitandao ya simu
badala ya kujingiza katika matumizi yasiyo sahihi ambayo yamekuwa
yakichangia kwa kiwango kikubwa kuondoa maadili katika jamii pamoja na
uchochezi.
Amesema kuwa sheria ya makosa ya mitandao nchini namba 14 inaweka
wazi juu ya adhabu atakayo weza kutolewa dhidi ya mtu au kikundi
kitakacho husika na upotoshwaji wa aina yoyote .
Amesema sheria ya makosa ya mitandao inaanisha makosa na adhabu
zinazohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na teknolojia ya habari
na mawasilino.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa wa mbeya ametumia fursa hiyo kulitaka
baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA- TCCC
kuendelea kuhamasisha ,kuelimisha pamoja na kutambua na kuelewa kero na
matalajio ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa
huduma za mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo ametoa wito kwa Makampuni
yote yaliyojikita katika uwekezaji wa mawasiliano ya simu ,huduma za
utangazaji na huduma za posta kuhakikisha wanaendelea kujenga mitandao
ya huduma zao nchi nzima ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika
maendeleo.
Aidha Mwenyekiti huyo ameviomba vyombo vya habari nchini kusaidia
kulitangaza Baraza hilo na shughuli zake ili wananchi wajue ni wapi pa
kupata ushauri na kutatua matatizo yao yanayohusiana na huduma za
mawasiliano.
Katika semina hiyo pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji Baraza pia
limeunda kamati ya watumiaji wa huduma za mawasililiano kwa mkoa wa
mbeya ambapo wajumbe wa kamati hiyo walichaguliwa kutoka miongoni mwa
wanasemina ambapo majukumu yao yatakuwa ni kuelimishajamii juu ya haki
wajibu na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko sanjali na kupokea toka
kwa watumiaji na kuyawasilisha kwa baraza.
No comments:
Post a Comment