Manispaa
ya Ilala Dar es Salaam nako wameshindwa kuchagua Meya na Naibu Meya
baada ya baadhi ya madiwani kuamua kukiuka taratibu za uchaguzi kwa
kuamua kupiga picha kwa kutumia simu ya mkononi karatasi ya kupigia
kura.
Uchaguzi
huo ulitakiwa kufanyika jana saa nne lakini kutokana na kuibuka kwa
dosari hizo ambazo zilisababisha uchaguzi huo kuahirishwa.Baada ya
kuahirishwa kwa uchaguzi huo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala ambaye
alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi John Ngonyani alisema wameamua kusitisha
uchaguzi huo hadi kesho (leo), saa nane mchana kwasababu ya baadhi ya
taratibu kukikuwa.
Pia
Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Dar es Salaam Mashauri Mussimu alistoa
ufafanuzi wa vipengele vya sheria ya uchaguzi huo ambapo alisema
uchaguzi huo utakuwa wa siri kulingana na muongozo.
Baada
ya ufafanuzi huo, Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema), alisimama
na kuomba muongozo ambapo alitaka uchaguzi huo uwe wa wazi na si
kufanyika kwa siri.
Madiwani wa Chadema wakati wanapiga kura hizo waliamua
kuoneshana nani ambaye amepigiwa kura na hapo ndipo ilipoanza kuibua
maswali miongoni mwa wajumbe wa uchaguzi huo.
Wakati
kwa madiwani wa CCM wao waliunga mkono mongozo wa kikao hicho kuwa kura
iwe ni siri ya mpiga kura.Hata hivyo hakukua na maelewano na ndipo
ilipoamriwa uchaguzi huo kuahirisha ambapo kabla ya uamuzi huo
wasilitisha kikao kwa muda kwenda kupata muafaka lakini ikashindakana.
Wapambe
wa CUF na Chadema waliokuwa kwenye eneo hilo la ukumbi waliamua kuzomea
madiwani wa CCM hasa kwa kuzingatia mbali ya kutakiwa kufanya uchaguzi
wa meya na Naibu Meya kulifanyika tukio la kuapisha madiwani ambapo
wengi wao walikuja na wafuasi wao.
Baadhi
ya Madiwani kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila
kiapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama Wilaya ya Ilala Mhe: Adelf
Sachore (hayupo pichani) kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam (wakwanza kushoto), Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala
Jimbo la Ukonga, Mhe: Tickey Kitundu (kulia katikati), Diwani wa Kata ya
Kariakoo, Mhe: Abdulkarim Masaki.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON
Madiwani
wakijaza fomu ya kiapo wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Viti Maalum
Wilaya ya Ilala Jimbo la Ukonga, Mhe: Tickey Kitundu.
Madiwani wakijaza fomu ya kiapo.
Hakimu
Mkazi wa Mahakama Wilaya ya Ilala Mhe: Adelf Sachore akiwaapisha
Madiwani (hawapo pichani), kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na
Segerea kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa walioudhuria wakishuhudia Madiwani wakila kiapo.
No comments:
Post a Comment