Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, anatarajiwa kuanza kambi nzito jijini Arusha kuanzia keshokutwa (Jumatano) kwa nia ya kuhakikisha kuwa mgombea ubunge wa chama chake katika katika Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema anatetea kiti chake kwa ushindi wa kishindo.
Taarifa
ambazo tulizipata jana toka kwa watu wa karibu wa Lowassa zilieleza
kuwa (Lowassa) ataungana na timu ya kampeni ya Chadema kujichimbia
jijini Arusha kwa siku zote zilizobaki za kampeni kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi huo Jumapili ijayo.
Uchaguzi
wa kumpata Mbunge wa Arusha Mjini haukufanyika Oktoba 25, 2015 kama
ilivyokuwa kwa majimbo mengine nchini kufuatia kifo cha mgombea wa
ACT-Wazalendo, Estomiah Mallah.
Kadhalika,
ilielezwa kuwa hatua hiyo ya Lowassa ni muendelezo wa ushiriki wake
katika kuiimarisha Chadema kwa nia ya kuleta ukombozi wa kweli kwa
Watanzania.
Hivi
karibuni alikuwa Mwanza na Geita kwa siku kadhaa katika kushughulikia
mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita, Alphonce
Mawazo, ambaye aliuawa kinyama na watu wasiojulikana.
Katika
hatua nyingine, Lema anayegombea kutetea jimbo hilo,alisema ushindi
kwake na chama chake uko wazi kwani wananchi wameamka na wengi wamepania
kumrejesha madarakani.
Alisema
kampeni zake za nyumba kwa nyumba ndizo zinazomuongezea uhakika wa
kushinda kwani hupokewa vizuri na wote humuahidi kujitokeza kwa wingi
Jumapili ili kumchagua.
Akizungumza
katika mkutano wake wa kampeni jana, Lema alisema atakapochaguliwa,
kazi kubwa atakayoifanya ni kuhakikisha kuwa mapato ya Halmashauri ya
Jiji yanaongezeka ili kufanikisha dhamira ya kuboresha huduma za jamii
kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment