Mbunge
wa Ubungo, Saed Kubenea (44) amekana kumtukana Mkuu wa wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda tarehe 14 Desemba 2015 walipokutana katika
Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd. kilichopo eneo la External Mabibo
kwa madhumuni ya kutatua mgogoro kati ya wafanyakazi na uongozi wa
kiwanda hicho
Katika
kesi inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Wakili
wa Serikali mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa alimsomea mshtakiwa maelezo
ya kesi hiyo ambapo baadhi ya mashtakiwa aliyakana.
Akisomewa
maelezo ya kesi, Saed Kubenea alikiri kuwa ni mbunge wa Ubungo na pia
alikiri kuwa anamfahamu mlalamikaji katika kesi hiyo kuwa ni Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Makonda na kwamba ni kweli kuwa tarehe 14 Desemba
2015 alifika katika Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd kulikokuwa na
mgomo wa wafanyakazi.
Hata
hivyo, alipoelezwa kuwa anashtakiwa kwa kosa la kumtolea lugha chafu
Makonda ambapo alimwita kuwa ni kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo chake
ni cha kupewa kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani na
utulivu; Saed Kubenea alikana.
Kufuatia
Kubenea kukana mashitaka yanayomkabili, Hakimu mkazi mkuu wa mahakama
hiyo , Thomas Simba alisema mashahidi sita wa upande wa mashtaka
wataanza kutoa ushahidi wao Januari 20 na 21, 2016 katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu.
No comments:
Post a Comment