Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi atembelea karakana kutengenezea breakpad za
vichwa vya treni kinachomilikiwa na kampuni miliki ya rasilimali za
Reli(RAHCO) leo asubuhi jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka (wa nne kutoka
kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasilimali
za Reli (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito, wakati akimwelezea namna
karakana ya kutengenezea breakpad za vichwa vya treni kilivyokuwa
kinafanya kazi, na sasa hakifanyi kazi, wakati Katibu Mkuu huyo
alipotembelea kiwanda hicho leo asubuhi, Katibu Mkuu ameipa wiki mbili
kampuni hiyo na Shirika la Reli Tanzani (TRL) kuuanda timu na kufanya
tathmini ya mitambo iliyoharibika na kuhakiki kiwanda hicho kinaanza
kufanya kazi.
Jengo
ambalo lilikuwa likitumika kama karakana ya kutengenezea breakpad za
vichwa vya treni, linavyoonekana baada ya kusitisha uzalishaji wa
breakpad hizo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa maelekezo kwa
uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mara baada ya kutembelea eneo
la Reli sehemu ya Malindi leo asubuhi.
Reli ambazo hutumika kubadilisha baada ya ziliyopo kuchakaa, zikiwa kwenye eneo la Malindi, kama zilivyokutwa leo asubuhi.
(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi).
No comments:
Post a Comment