JAJI Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama alishinda atashinda tena kutokana na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa watampIgia kura tena.
Boman
aliyasema hayo jana jijini Dar eS Salaam , wakati akizungumza na
waandishi wa habari.Alisema kuwa Maalim kujitangazia kuwa ameshinda ni
suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo kutokana na mazingira hayo
uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya Zanzibar.
“Kurudia
uchaguzi Zanzibar ni jambo lisilo epukika lakini wakae na kuangalia
dosari zilizojitokeza na kufuta uchaguzi ili lishughukiwe kisheria,
bila kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo” alisema Jaji Mstaafu, Boman.
Alisema
kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar walitakiwa kukaa na kuona wapi
walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo ilikuwa ngumu kutokana
na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha na wajumbe
walishindwa kuafikiana.
Kuhusu suala la katiba
mpya, Bomani alisema ni lazima lishughulikiwe kuanzia pale lilipoishia
kwani kuachwa kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni ya fedha yaliyotumika katika mchakato huo.
Alisema migogoro ya wafugaji na wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo ndio ingekuwa suluhu ya utatuzi wa migogoro hiyo.
No comments:
Post a Comment