Mmoja wa wagombea
wa kiti cha Urais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Mosima Gabriel
"Tokyo" Sexwale raia wa Afrika Kusini, amehojiwa kuhusiana na madai ya
ufisadi wakati wa maandalizi ya mashindano ya kombe la dunia.
Tokyo
Sexwale amefika mbele ya majaji wa Marekani katika jiji la New York,
kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusiana na madai ya ulaji rushwa
ndani ya FIFA.Shirika la Habari la BBC linafahamu kuwa alihojiwa kuhusiana malipo ya dola milioni kumi($10m) malipo iliyotolewa kwa njia ya yenye utata na taifa la Afrika Kusini kwa naibu rais wa zamani wa Fifa Bwana Jack Warner.
Sexwale amefika huko kama shahidi muhimu baada ya shirika la upelelezi la Marekani FBI kumtaka kufika mbele ya majaji Desemba 17.
Alikuwa mojawepo wa wanachama wa halmashauri kuu iliyokuwa inapigia debe Afrika Kusini kupewa uwenyeji wa maandalizi ya mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010.
Madai ya Marekani kwamba pesa hizo alilipwa Warner kupitia akaunti ya FIFA, na kufichwa kama pesa za kukuza soka, ili kupata kura nyingi zaidi kwa Afrika Kusini kupata zabuni ya uwenyeji wa kuandaa mashindano hayo.
Msemaji wa Sexwale ameiambia BBC kuwa "kwa kweli alifika mbele ya majaji hao. FBI inasema kuwa alitakikana kufika huko, na alienda kama shahidi muhimu."
Sexwale ni mmoja kati ya wagombea kiti cha Urais wa FIFA, katika uchaguzi unaopangiwa kufanyika Februari 26 hapo mwakani.
No comments:
Post a Comment