WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Joyce Ndalichako, amesema atafuatilia shule za Serikali ili kujua sababu za kufanya vibaya katika mitihani yao.
Dk Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), amesema hayo jana baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli, kushika wadhifa huo.
“Kwa
kuwa lengo langu ni kuona elimu bora inatolewa, nitafuatilia kujua
sababu ya shule maalumu za Serikali kushuka kiwango chake katika ufaulu
wa mitihani,” alisema.
Kwa mujibu wa Dk Ndalichako, shule hizo za Serikali hasa za vipaji maalum, ndizo awali kila mwanafunzi alipenda kwenda kusoma tofauti na sasa ndio maana anataka kujua kulikoni.
Kwa mujibu wa Dk Ndalichako, shule hizo za Serikali hasa za vipaji maalum, ndizo awali kila mwanafunzi alipenda kwenda kusoma tofauti na sasa ndio maana anataka kujua kulikoni.
Shule hizo ni pamoja na Mzumbe, Ilboru, Tabora Wavulana, Tabora Wasichana, Kilakala na Msalato.
Wanaoongeza Ada Kiholela Kukiona
Kuhusu upandaji holela wa ada za shule binafsi, Dk Ndalichako alisema atapambana na vyuo vikuu na shule binafsi, zinazofanya ujanjaujanja wa kupandisha ada tofauti na ile iliyoandikwa kwenye barua za kuwaita wanafunzi, jambo linalosababisha usumbufu kwa wazazi.

Alisema
lengo lake ni kuhakikisha Tanzania inatoa elimu bora kwa wahitimu wa
vyuoni na sekondari, itakayowawezesha kukidhi soko la ajira la
kimataifa.
Pamoja na ubora huo, Dk Ndalichako alisema ataangalia uwepo wa miundombinu kwa wanafunzi wa kuanzia shule ya msingi na sekondari, ambako alikiri kuwa baadhi ya wanafunzi wanaketi chini na wengine wana matatizo ya mashimo ya vyoo.

“Inakuwaje
shule yenye maelfu ya wanafunzi watumie shimo moja la choo, haya na
mambo mengine yanakwaza wanafunzi wasipende shule na wengine wakatize
masomo yao.
“Tunataka kuandaa mwanasayansi, hivi kweli mwanafunzi anayeketi chini anaweza kuwa mtaalamu mzuri wa sayansi? Ni lazima tuwezeshe shule zetu ziwe na miundombinu rafiki kwa wanafunzi,” alisema Dk Ndalichako.

Pia
alisema atashughulika na tatizo la baadhi ya vyuo kutoa kozi zinazoenda
kinyume na ithibati walizopewa na mamlaka za elimu, jambo linalofanya
wanafunzi wanaosoma kwenye vyuo hivyo kutotambuliwa na waajiri.
No comments:
Post a Comment