Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Tukio
hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa
kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa
Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua
jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert.
Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya.
Wakati
akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia
anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza
gemu la Bongo Fleva vibaya.
Hata
hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia
wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond
naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.
Kufuatia
hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa
Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na
kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia
machozi kaka yake huyo.
Diamond
alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen,
meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada
kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake.
Kwa hiyo anyamaze.
Licha
ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea
kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa
kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara
ndani yake.
“Huna
sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa
na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza
kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.
Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!
Kilio
hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada
ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku
hiyo katika kumbukumbu.
Wimbo ulimuliiza Diamond huu hapa
Wimbo ulimuliiza Diamond huu hapa
No comments:
Post a Comment