CHAMA
cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimetishia kuwaondoa wahasibu waliokuwepo
kwenye daftari la chama hiko endapo watakiuka taratibu na maadili ya
kazi kulingana na matakwa ya chama hicho ikiwemo ya rushwa, wizi na
ufisadi.
Hayo
yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Fred
Msemwa katika mazungumzo yake na wanahabari wakati akitoa pongezi na
kuunga mkono kwa jitihada za serikali ya awamu ya nne juu ya ukusanyaji
wa mapato.
Msemwa
alisema kuwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu, wanatakiwa kufanya kazi
kwa mujibu wa taaluma zao kwa kufuata miongozo ya sheria Na.33 ya 1973
inayosimamia taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu Tanzania.
Amesema
kuwa chama hicho hakitasita kumundoa mhasibu yoyote atakayeshiriki
katika wizi na mambo mengine kinyume na matarajio ya wananchi
ataondolewa haraka.
No comments:
Post a Comment