Baada ya stori nyingi kuingia katika headlines kwa siku za hivi karibuni kuhusu uamuzi wa moja kati ya mabilionea wa Afrika kutaka kuinunua klabu ya Simba, mengi yameandikwa na mengi yameongewa. kuhusu Mohamed Dewji maarufu kama MO ambaye amewahi kutajwa na jarida la Forbes kuwa ni bilione wa 24 Afrika kutaka kuinunua Simba.
Ikiwa ni wiki moja imepita toka uongozi wa Simba kupitia kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara atangaze kuwa stori za MO kutaka kuinunuaSimba zinatajwa tu katika vyombo vya habari lakini bado bilionea huyo hajaandika barua rasmi ya kuomba kuinunua Simba.
December 29 imetoka statement yake kuwa Mohamed Dewji ambaye anadai kufanya majadiliano na viongozi hao kwa zaidi ya miezi miwili, amechoka na kutopewa majibu ya kutoeleweka, kwani hadi sasa amekutana na Rais wa Simba Evans Aveva na viongozi wengine ila hakuna majibu. Hivyo uamuzi wake ni kuwa katoa siku tatu kuanzia December 29 hadi 31 2015 viongozi watoe jibu la kukubali au kukataa.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mohamed Dewji ‘MO’ ambaye anataka kuinunuaSimba kuiendesha kibiashara kwa kuwekeza bilioni 20 za kitanzania, mwezi March 2015, alitajwa na jarida la Forbes la Marekani kuwa moja kati ya mabilionea 29 wa Afrika akiwa nafasi ya 24 kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1.3 ambazo ni sawa na Tsh trilioni 2.34.
No comments:
Post a Comment