Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza wakati
akifungua rasmi Mkutano wa siku mbili wa Asasi za Kiraia kutoka Nchi za
Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Jijini
Dar es Salaam. Mkutano huo uliwashirikisha wenyeviti wa asasi za kiraia
kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu.
Sehemu ya Wajumbe wakifuatilia ufunguzi wakati Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akizungumza (hayupo pichani)
Sehemu nyingine ya wajumbe wakifuatilia ufunguzi.
Wajumbe wengine wa mkutano.
Mwenyekiti
wa Asasi za Kiraia eneo la Maziwa Makuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku akizungumza wakati wa
mkutano huo.
Wajumbe wakifuatilia wakati Mzee Butiku akizungumza.
Balozi Mulamula akiagana na Mzee Butiku mara baada y akufungua mkutano.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Samwel Shelukindo akizungumza na mmoja wa washiriki wa mkutano mara baada ya ufunguzi.
Balozi Mulamula akizungumza na Wandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa Asasi za Kiraia katika eneo la Maziwa Makuu.
Picha ya Pamoja kati ya mgeni rasmi Balozi Mulamula na Wajumbe wa Mkutano
=================================
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa Asasi za
Kiraia zina nafasi kubwa katika utatuzi wa migogoro na kuleta amani
hususan katika eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu na Afrika kwa ujumla.
Balozi
Mulamula aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa Wenyeviti wa
Asasi za Kiraia kutoka Nchi za Maziwa Makuu unaofanyika kwa siku mbili
katika Hoteli ya Golden Tulip, Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Mulamula ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Kwanza wa
Sekretarieti ya Maziwa Makuu alisema kuwa kwa uzoefu wake utatuzi wa
migogoro, kulinda amani na katika kuhakikisha demokrasia na utawala wa
sheria vinafuatwa kila chombo kina nafasi na umuhimu wake na kwamba
Asasi za Kiraia zina nafasi kubwa zaidi kwani zinawakilisha maoni ya
wananchi.
“Asasi
za Kiraia ni chombo muhimu sana katika kuhakikisha amani inakuwepo
hususan katika Ukanda wa Maziwa Makuu kwani zinawawakilisha wananchi
moja kwa moja hivyo ni vizuri kutambua nafasi yenu”, alisema Balozi
Mulamula.
Aidha,
aliipongeza Asasi hiyo ya ambayo kwa kiasi kikubwa imefanikiwa tangu
ilipoanzishwa mwaka 2011 na kusisitiza ijikite zaidi katika kutekeleza
majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha misingi ya demokrasia,
utawala bora na utawala wa sheria katika nchi za Ukanda wa Maziwa makuu
vinafuatwa na kutekelezwa kikamilifu.
“Najua
mnazijua hadidu za rejea na wajibu wenu kama Asasi za Kiraia, ni
kuhakikisha nchi wanachama zinafuata misingi ya sheria, utawala bora na
ule wa sheria ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara katika eneo letu la
Maziwa Makuu”, alisisitiza Balozi Mulamula.
Awali
akimkaribisha Balozi Mulamula kuzungumza, Mwneyekiti wa Mkutano huo
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph
Butiku alisema kwamba mkutano huo wa Wenyeviti wa Asasi kutoka nchi
wanachama wa Maziwa Makuu ni muhimu sana hususan katika kipindi hiki
ambapo pamoja na mambo mengine utaandaa na kupitisha agenda za Asasi
hiyo zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi unaotarajiwa
kufanyika mwezi Februari, 2016.
Aidha,
aliongeza kuwa wakati umefika kwa Nchi Wanachama wa Maziwa Makuu
kutambua mchango wa asasi za kiraia na kuzishirikisha ipasavyo katika
msuala muhimu hususan yale ya utatuzi wa migogoro ili kuleta tija kwenye
eneo hili la Maziwa Makuu ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa na migogoro
ya kisiasa na kikabila.
Mkutano
huo wa siku mbili uliwashirikisha Wenyeviti wa Asasi kutoka nchi zote
12 wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda,
Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Rwanda, Jamhuri ya Congo, Angola, Sudan na Zambia.
No comments:
Post a Comment