Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wake, Mhe.
Dkt. Suzan Kolimba waliwasili Wizarani kuanza kazi rasmi siku ya
Jumamosi tarehe 12 Desemba 2015.
Viongozi
hao wapya wa Wizara walipokelewa na watumishi kwa shangwe walipowasili
wizarani, muda mfupi baada ya kula kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Dar
es Salaam.
Siku
ya kwanza Wizarani, Waheshimiwa Mawaziri walipata fursa ya kukutana na
uongozi wa Wizara ukiongozwa na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula na
Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi.
Joyce Mapunjo. Makatibu Wakuu hao pamoja na mambo mengine, walikabidhi
kwa Waheshimiwa Mawaziri nyaraka muhimu za Wizara zitakazowaongoza
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha,
walitumia fursa hiyo kueleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara na
masuala ambayo yanahitaji miongozo yao ili yaweze kufanyiwa kazi na
kukamilishwa.
Balozi
Mahiga na Dkt. Kolimba walipata fursa pia ya kutembelea watumishi wa
iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki siku ya tarehe 14
Desemba 2015 kwenye Jengo la Waterfront. Watumishi hao kama walivyofanya
wenzao waliwapokea viongozi wapya kwa shangwe na baadaye kufanya kikao
na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Katika
vikao vyote, Mhe. Waziri aliomba ushirikiano kutoka kwa Wakuu wa
Idara/Vitengo na watumishi wote kwa jumla ili kwa pamoja waweze kuendana
na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye kaulimbiu ya
“Hapa kazi tu”
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula aliyesimama akitoa neno kabla ya kumkaribisha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) kuongea na Wakuu wa Idara/Vitengo wa Wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba |
|
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi,
Bw. Wilfred Masanja (wa kwanza kulia), na Kaimu Mkuu wa Idara ya Sera
na Mipango, Bw. John Ngowo wakisikiliza kwa makini neno la ukaribisho kutoka kwaBalozi Mulamula akimkaribisha Mhe. Waziri kuzungumza na Wakuu wa Idara/Vitengo. |
|
Sehemu
nyingine ya Wakurugenzi walioudhuria kikao hicho, wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw.
Negel Msangi, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Balozi Anisa Mbega
(katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi
Innocent Shiyo. |
|
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga
(wa kwanza kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki Bi. Grace
Martine (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya,
Bi. Tunsume Mwangolombe (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Eva Ng'itu nao wakiwa kwenye
mkutano wa Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Dkt. Kolimba (hwapo
pichani). |
|
Sehemu
nyingine ya Viongozi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Afrika, Balozi Samuel Shelukindo, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi
wa Ndani Bw. Marthias Abisai (wa kwanza kushoto), na Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha TEHAMA Bw. Nassoro Msumi (katikati). |
|
Kikao kikiendele ========Kikao na Uongozi wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki======== |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kutoka kushoto), na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzani Kolimba (wa kwanza kushoto)
wakimsiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Bi. Joyce Mapunjo (wa pili kutoka kulia) katika kikao baina ya Mhe. Waziri na Wakuu wa Idara na Vitengo, wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mwingine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Amantius Msole. |
|
Mhe. Joyce Mapunjo akiwatambulisha Wakurugenzi wake (hawapo pichani) kwa Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Waziri Kolimba |
|
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Ulinzi na Siasa Bw. Amani Mwatonoka
akijitambulisha kwa Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Waziri Dkt. Kolimba
(hawapo pichani). |
|
Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wakifuatilia kwa makini kikao kilichokuwa kinaendelea. |
|
Makatibu
wa Mawaziri nao wakifuatilia kwa makini mkutano huo, wa kwanza kushoto
ni Bw. Thobias Makoba, na Adam Isara (wa kwanza kulia). |
|
Kikao kikiendelea |
No comments:
Post a Comment