Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya miaka 45 ya
Taifa la Oman yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Oman hapa nchini na kufanyika
kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) tarehe 24 Novemba, 2015.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali akiwemo
Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Salim
Ahmed Salim. Katika hotuba yake Balozi Yahya alisifu uhusiano wa
kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Oman na kuitakia heri nchi hiyo
katika kuadhimisha miaka 45.
Balozi
wa Oman hapa nchini, Mhe. Soud Al Mohammed Al-Ruqaish akitoa neno la
shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 45 ya Taifa
la Oman. Pia alisifu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi yake na
kuahidi kuuendeleza na kuuimarisha.
Mhe.
Mwinyi (wa kwanza kushoto) kwa pamoja na Mhe. Salim (wa pili kushoto)
na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf (wa pili
kulia) wakiwa kwenye sherehe hizo pamoja na wageni wengine waalikwa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (kulia) akiwa na Afisa
Mambo ya Nje, Bw. Tahir Khamis (mwenye suti ya kijivu) pamoja na wageni
mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya Miaka 45 ya Taifa la Oman.
Kiongozi
wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Balozi Juma Halfan Mpango
(kushoto mwenye suti ya kijivu) akiwa na Balozi wa Burundi hapa nchini,
Mhe. Issa Ntambuka wakati wa maadhimisho ya sherehe ya miaka 45 ya Taifa
la Oman.
Balozi
wa Oman, Mhe. Al-Ruqaish akiwaongoza Viongozi Wastaafu, Mabalozi na
Mgeni rasmi Balozi Yahya kukata keki kama ishara ya kusherehekea siku
hiyo kubwa kwa Taifa la Oman.
Wageni
waalikwa wakifuatilia sherehe hizo akiwemo Afisa Mambo ya Nje kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Batholomeo Jungu
(mwenye suti ya kijivu).
Maafisa
Mambo ya Nje wakifuatilia sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman. Kutoka
kulia ni Bw. Ali Ubwa, Bw. Seif Kamtunda na Bw. Hangi Mgaka.
Mhe. Mwinyi akijadili jambo na Mhe. Salim kabla ya kuanza kwa sherehe hizo za miaka 45 ya Taifa la Oman.
Picha ya Juu na Chini ni Sehemu ya Wageni waalikwa wakati wa sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman.
Sehemu nyingine ya Wageni waalikwa.
Wageni waalikwa.
No comments:
Post a Comment