WATUMISHI WANNE HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI WASIMAMISHWA KAZI NI BAADA YA KUBAINIKA KUKWAPUA ZAIDI YA MILIONI 70 - LEKULE

Breaking

13 Nov 2015

WATUMISHI WANNE HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI WASIMAMISHWA KAZI NI BAADA YA KUBAINIKA KUKWAPUA ZAIDI YA MILIONI 70

HALMASHAURI ya wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.

Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha  mfukuza kazi.

Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi  waliostaafu  na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na wananchi alipofanya ziara katika hosptali teule ya Machame na kuzungumza na wafanyakazi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya viongozi wa Hosptali hiyo na viongozi wa serikali wa wilaya ya Hai.
Baadhi ya wafanyakazi.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi katika hosptali ya Machame ,Dkt Fredrick Muro akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya watumishi wa Hosptali hiyo.
Baadhi ya madktari wa hosptali teule ya Machame.

Mkuu wa wilaya akiondoka katika hosptali hyo mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi.

No comments: