Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto),
akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja ,
wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini jijini Dar
es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Sylvester Ambokile.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto), akimuonesha Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya
Ofisi za Idara ya Uhamiaji, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara
katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye
tai),akipewa maelezo alipotembelea Dawati la Mapokezi wakati wa ziara ya
kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,Kurasini, jijijni
Dar es Salaam.
Afisa
Uhamiaji, Lilian Maleko akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai), jinsi taarifa za
muombaji pasi ya kusafiria zinavyohakikiwa, wakati wa ziara ya kikazi
Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Afisa
Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa hati za kusafiria, Amir
Hassan (wa pili kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),moja ya pasi iliyokua
imeshachapwa tayari kwa matumizi ya kusafiria, wakati wa ziara ya kikazi
Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Kamishna
wa Uhamiaji (Vibali vya Ukaazi, Visa na Pasi), Victoria Lembeli
(katikati), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, John Mngodo, moja ya karatasi iliyokataliwa na mfumo wa komputa
baada ya kubainika kwa taarifa za uongo za muombaji wa Hati ya Ukaazi,
wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji,
Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Maafisa
wa Idara ya Uhamiaji, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (hayupo pichani), alipofanya mkutano
nao wakati wa ziara aliyofanya Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini,
jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Silvester Ambokile akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya machapisho
ya Idara ya Uhamiaji, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Makao
Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye
tai) katika picha ya pamoja na viongozi wa Idara ya Uhamiaji wakati
alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es
Salaam. Wapili kushoto mstari wa mbele, ni Mkurugenzi wa Utawala na
Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bi.
Lilian Mapfa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment