Washiriki wa shindano la Bongo style kwa upande wa picha wakimsikiliza kwa makini mtaalam wao Sameer Kermalli(wa tatu kulia) akitoa maelekezo wakati wa mafunzo hayo.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande akiwa na washiriki wa shindano la Bongo Style ambao hawapo pichani , akiwa na Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alipofika kuwatembelea na kuongea nao machache.
Baadhi ya Washiriki kwa upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanachakalika kuandaa kazi zao mbalimbali
Mbunifu wa Mavazi Martini Kadinda akiwapa somo washiriki upande wa ubunifu wa mavazi.
Hawa
ni washiriki kwa upande wa kupiga picha wakikamilisha moja ya mazoezi
waliyopewa(Picha kwa hisani ya Washiriki upande wa wapiga picha)
Baadhi ya Washiriki upande wa kupiga picha wakiwa mtaani wakiwa katika mazoezi waliyopewa kuyafanya na mtaalam wao Sameer Kermalli
Baadhi
ya washiriki wengine kwa upande wa Kupiga picha na ubunifu wa mavazi wakisikiliza kwa makini
somo ambalo linatolewa na mtaalam ambaye hayupo pichani.
Baadhi
ya washiriki upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanasikiliza kwa makini
maelekezo wanayopewa na Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda ambaye hayupo
pichani
Muda wa mapumziko
Muwezeshaji kutoka Wiki Loves Africa akitoa somo juu ya upigaji picha kwa washiriki ambao hawapo pichani.
Tunukiwa Daudi (Aliyesimama) akitoa somo juu ya matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na Faida zake
Baadhi ya washiriki upande wa kupiga picha wakifurahia jambo
Ikiwa
ni siku ya tano tangu Washiriki 20 wa Shindano la Bongo Style linalo
andaliwa na asasi isiyo ya Kiserikali ya Faru Arts and Sport
Development Organization (FASDO), ikiwahusha Wapiga picha na wabunifu wa
mavazi wenye umri kati 19-25 walioingia rasmi kambini tarehe
5.11.2015,ambapo tangu tarehe hiyo washiriki hao
wameendelea kujifua zaidi huku wakipewa kazi mbalimbali za ubunifu na
masomo mengine ikiwa ni sehemu ya shindano hilo. Wakiwa kambini washiriki hao wamepata nafasi ya kujifunza mambo mapya ambayo walikuwa hawayafahamu.
Fainali hizi zinatarajiwa kufanyika tarehe 27.11.2015 ndani ya ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti washiriki wa upande wa picha wamekili kuwa walikuwa
wanaona kama wanafahamu vema kupiga picha lakini baada ya kupata somo
wamegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu na mengine
walikuwa wanayafanya lakini bila kujua kuwa walikuwa sahihi, Pia
waliongeza kuwa wanashukuru kuwapata wataalam ambao wameweza kuwaonesha
ni jinsi gani wanatakiwa kuwa wapiga picha wazuri.
Nao
washiriki wa ubunifu wa mavazi wameshukuru kupata wataalam ambao
wamekuwa wakiwapa maelekezo mengi ambayo yalikuwa ni chachu kwao
kwasababu kila mmoja kwa upande wake wamejifunza mambo mapya mengi na
kuona kuwa kumbe sio lazima kuwa na ubunifu wa aina moja ya mavazi
lakini wanaweza wakawa na aina nyengine nyingi kulingana na mazingira
waliyopo na kuishukuru Fasdo kwa kuwakutanisha.
Mwalimu na mtaalam wa kupiga picha Sameer Kermalli amekili kuwa tangu darasa lianze washiriki hao wamekuwa na uelewa wa haraka na yeye kupata nafasi ya
kuwaelekeza mbinu mbalimbali za kupiga picha na kanuni mbambali za
upigaji picha, washiriki hao wamekuwa wasikivu na wameongeza ubunifu
zaidi jambo ambalo limemtia moyo mtaalam huyo.
Kwa
upande wa Mbunifu wa mavazi Martin kadinda alisema kuwa washiriki wapo
vizuri na kila mbunifu anakitu chake cha kipekee ambacho yeye anafanya
mfano wapo wale ambao wanabuni nguo zao kwa kutumia kitenge tu, wengine
wanatumia vitu vya asili, nguo za kisasa, nguo ambazo zipo tayari kwa
ajili ya kuvaliwa na zenginezo, aliwashauri kuwa wasiegemee katika kitu
kimoja tuu au aina moja ya mavazi lakini wawe na ubunifu na kubadilika
kila wakati kwa sababu mitindo inakwenda ikibadirika.
Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande alipata nafasi ya kutembelea kambini na kujionea jinsi washiriki wanavyojituma katika kazi zao na maandalizi ya shindano hilo yanavyo kwenda " Ninachukua nafasi hii kwa niaba ya Fasdo kuwapongeza washiriki wote mliofanikiwa kuingia katika shindano hili la Bongo style ikiwa lengo ni kuwajengea uwezo zaidi wa kile ambacho mlikuwa mnafanya na sasa kipate kuwa zaidi" aliongea Chande na kuongeza kuwa kuna ushindani mkubwa na shindano linafuata vigezo vyote vya ushindani na washindi watakuwa wamekidhi vigezo hivyo.
No comments:
Post a Comment