Wanafunzi
wa shule ya msingi Chazinge A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani
wamenufaika kwa kupatiwa msaada wa vifaa vya elimu kutoka taasisi ya
kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation.Vifaa hivyo ambavyo
vimetolewa jana ni madaftari ya kuandikia na mikebe yenye vifaa vya
kusomea somo la hisabati (Mathematics set)pamoja na kalamu.
Akiongea
wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa hivyo kwa wanafunzi jana,Kaimu
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn
Mworia alisema elimu ni moja ya kipaumbele ambacho taasisi hiyo inatoa
na vipaumbele vingine vikiwa ni kusaidia kuboresha sekta ya afya.
“Vodacom
Foundation tunaelewa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na hakuna jamii
ambayo inaweza kuendelea bila kutoa elimu kwa watu wake ndio maana
tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha
sekta ya elimu nchini”.Alisema Mworia.
Alisema
kuwa taasisi ya Vodacom Foundation pia inaendelea kutekeleza mkakati
wake wa kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hususani
zile zinazomilikiwa na serikali wanapatiwa kompyuta za kuwawezesha
kusoma somo hili kwa vitendo ili wasiachwe nyuma katika karne hii ya
sayansi na teknolojia.
Akiongea
kwa niaba ya wanafunzi wenzake baada ya kupokea msaada huo mwanafunzi
Aisha Salum anayesoma darasa la nne shuleni hapo alitoa shukrani kwa
msaada huo “Tunashukuru Vodacom Foundation kwa kutupatia vifaa na tuna
imani vitatusaidia katika masomo yetu.
Mwanafunzi
wa darasa la sita Jonson Khamsini (wa pili toka kushoto) wa shule ya
Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani akipokea vifaa
vya elimu-madaftari,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati
(Mathematics set) pamoja na kalamu toka kwa Kaimu Ofisa Mkuu wa
Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kulia)
ikiwa ni msaada ulitolewa na kampuni hiyo kupitia taasisi ya kusaidia
masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Kaimu
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn
Mworia(kulia)akimkabidhi Mariam Yusuf msaada wa vifaa vya
elimu,madaftari,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati
(Mathematics set)ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya
Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.Msaada huo
ulitolewa na kampuni hiyo kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya
jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe
mkoani Pwani,wakigawiwa vifaa vya elimu na Kaimu Ofisa Mkuu wa
Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kulia)
vikiwemo,madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la
hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na kampuni hiyo
kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation
hivi karibuni.
Meneja
Biashara wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha Vodacom Tanzania,
Grace Lyon (kulia) akiwagawia vifaa vya elimu wanafunzi wa shule ya
Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani, vifaa
walivyokabidhiwa ni,madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo
la hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na kampuni
hiyo kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom
Foundation hivi karibuni.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe
mkoani Pwani,wakifurahia na kuviinua juu vifaa vyao vya elimu,
Vikiwemo,madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la
hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na Vodacom
Tanzania kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom
Foundation hivi karibuni.
Wanafunzi
wa darasa la sita katika shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani
Kisarawe mkoani Pwani,Jonas Mkwagi (kushoto) na Khamis Haji(kulia)
wakishirikiana na Meneja wa Vodacom Foundation,Sandra Oswald (katikati)
kubeba boksi lenye vifaa vya elimu vikiwemo madaftari,kalamu,Mikebe
yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) ikiwa ni
msaada uliotolewa na Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya kusaidia
masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment