BENKI
ya Barclays hapa nchini yawaletea wapezi wa soka kombe la ligi kuu ya
uingereza kwaajili ya kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu ni mwisho wa
benki hiyo kudhamini ligi kuu nchini Uingereaza, Pia wananchi wajitokeze
kufungua akaunti kwaajili ya mshara katika benki hiyo ili kujishindia
tiketi mbili za kwenda kuangalia ligi kuu ya uingereza.
Hayo yamesemwa na Kaimu
Mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
"Wapezi
wa soka wajitokeze kwa mujibu wa ratiba ya benki a Barclays kwaajili ya
kugipatia picha wakiwa na kombe la benki hiyo ikiwa ni mwaka huu ni wa
mwisho kudhamini ligi kuu ya Uingereza iliyokuwa ikijulikana kama
Barclays Premier League." Bendera
Nae Mkuu
wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa amesema
kuwa Disemba 3 mwaka huu kombe hilo litaanzia katika tawi kuu la benki
benki hiyo Posta kuelekea Mwembe yanga kupitia
barabara ya Pungu mpaka Temeke Hospitali, Uwanja wa Taifa, kituo cha
magari cha Mombasa na kumalizia viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
Salaam.
Na
Disemba 4 litaanzia kutembezwa kutokea katika benki ya Barclays tawi la
Alpha kuelekea ofisi za IPP Media, Mlimani City, tawi la benki hiyo la
Slip way Kinondoni Biafra, Mazese Darajani na kuishia katika viwanja vya
Karume jijini Dar es Salaam.
Aidha Mwakyusa
aliyoa wito kwa wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupiga
picha na kombe la ligi kuu ya Uingereza ambapo mwaka huu ni mwisho wa
benki ya Barclays kudhamini ligi kuu Uingereza.
Mkuu
wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa na Kaimu
mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera wakiwa
wameshika picha ya kombe la mpira ambayo litatembezwa Disemba 3 na 4
mwaka huu jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapenzi wa mpira wa miguu
kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu benki ya Barclays ni mwisho wa
kudhamini ligi kuu uingereza.
Kaimu Mkuu
wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na benki hiyo
kutembeza kombe la Barclays premier ligi ya Uingereza kulitemeza jijini
Dar es Salaam kwaajili ya wapezi wa soka jijini hapa kupiga nalo picha
ambazo itakuwa kumukumbu kwao.Kusoto ni Grace Josef na kulia ni Rhobina
Justine wakiwa ni miongoni wa washiriki wa benki hiyo katika kutembeza
kombe hilo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza
na waandishi wa habari kuhuriana na ratiba ya kombe hilo litakavyokuwa
likizungushwa ili wapenzi wa soka kupiga picha na kombe ikiwa benki ya
Barclays ni mwaka wa mwisho kudhamini ligi ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment